Thursday, 28 April 2016
Majengo 20 ya CCM Kubomolewa Moshi.
Ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kinyume na sheria za mipango miji katika Manispaa ya Moshi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ubomoaji huo unakusudiwa kuambatana
na uvunjaji wa majengo zaidi ya 20 ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyopo katika Kata ya Mawenzi.
Meya wa manispaa hiyo, Raymond Mboya
amewaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kusimamia ipasavyo sheria hiyo ili kuhakikisha majengo yaliyojengwa kinyume na sheria yanavunjwa.
Mboya amesema sheria ni lazima ifuatwe
haijalishi ni chama gani kimejenga kinyume.
“Leo tunapata ugumu wa kuwa jiji kutokana na sisi wenyewe kushindwa kusimamia sheria za mipango miji, hatuwatendei haki wakazi wa Manispaa ya Moshi ni lazima ifike wakati watu
tujue kuna mamlaka ambayo imekabidhiwa kusimamia mji,”amesema Mboya.
Kwa upande wake Loth Ole Mesele, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini amesema hajapata taarifa hizo za kubomolewa kwa majengo ya chama hicho.
Magufuli amsimamisha kazi kisa hachukui mshahara.
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa
Mkurugenzi Mtendaji TIC, Bi Juliet Kaoruki ambapo pamoja na mambo mengine sababu ya Mh Rais. Kutengua uteuzi huo ni kutokana na kutochukua mshahara wa serikali.
Kadhalika Bi. Kairuki ameingia kwenye list ya watumishi kadhaa wa serikali waliosimamishwa kazi na kupewa ahadi ya kupangiwa kazi nyingine.
Kivuli cha taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo April,28 2016
Wednesday, 27 April 2016
Uhaba wa umeme wasababisha watumishi wa umma kufanya kazi siku kwa wiki Venezuela.
Serikali ya Venezuela imeagiza wafanyakazi
wake wawe wakifanya kazi siku mbili kwa wiki.Hii ni hatua ya muda iliyochukuliwa kutokana na uhaba wa umeme.
Makamu wa Rais Aristobulo Isturiz ametangaza kwamba watumishi wa umma wanafaa kufika kazini Jumatatu na Jumanne pekee hadi mzozo wa sasa wa nishati umalizike.
Venezuela imekabiliwa na ukame mkubwa ambao umepunguza maji kwenye bwawa lake kuu la kufulia umeme.
Lakini upinzani umeituhumu serikali kwa
kutodhibiti vyema mzozo wa sasa. Agizo la kupunguzwa kwa siku za kufanya kazi,
lililotolewa kupitia runinga ya taifa na Bw Isturiz.
"Hakutafanywa kazi katika sekta ya umma
Jumatano, Alhamisi na Ijumaa, ila tu majukumu muhimu sana.” alisema.
Amesema Venezuela imeathiriwa sana na hali ya hewa ya El Nino na kwamba hali ya kawaida itarejea baada ya mvua kuanza kunyesha.
Serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa
kupunguza matumizi ya umeme. Februari, maduka yaliagizwa kupunguza muda
ambao yanafunguliwa kila siku na pia kujaribu kujizalishia umeme.
Mapema wiki hii, serikali pia ilisongeza mbele saa kwa nusu saa ili kupunguza mahitaji ya umeme kwa ajili ya mwanga mapema jioni.
Tuesday, 26 April 2016
Mke Wa rais mstaafu wa Kenya afariki dunia Jumanne hii
FirstLady wa zamani wa Kenya Lucy Kibaki amefariki dunia Leo Jumanne.
Taarifa ya Rais Uhuru Kenyatta imedai kuwa Mrs Kibaki alifariki akitibiwa katika hospitali ya Bupa Cromwell ya London.
“Her excellency has been unwell for the last one month and has been receiving treatment here in Kenya and subsequently in the United Kingdom,” yamesema maelezo hayo.
Mrs Kibaki alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Nairobi mwezi uliopita baada ya kutafuta matibabu katika hospitali ya Gertrude ya Muthaiga.
Ameacha watoto wanne, Judy Wanjiku, Jimmy Kibaki, David Kagai na Tony Githinji.
Watatu wakamatwa wakisafirisha Madawa Kilimanjaro
Watu watatu akiwemo mmoja raia wa Kenya
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa
ya kulevya aina ya Mirungi na Bangi kilo 54
na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa
kutoka nchini Kenya kwenda mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro
Bw.Wilbrod Mutafungwa amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa katika
maeneo ya njia panda Himo wilaya ya Moshi
na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye
miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi
miguuni.
Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor
mfanyabiashara mkoani Arusha, Naftal Mvoyi
mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis
mkazi wa Arusha ambao walikuwa
wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia
magazeti na gundi ya karatasi na kisha
kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa
wakitokea nchini Kenya kuelekea jiji la
Arusha.
Ripota wetu amefanikiwa kuzungumza na
baadhi ya vijana wanaojihusisha na matumizi
ya madawa ya kulevya katika manispaa ya
Moshi na kueleza kwamba changamoto
kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali
inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na
matukio ya uhalifu.
Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri
vijana wengi kiafya kutokana na baadhi yao
kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na
hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya
wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Subscribe to:
Posts (Atom)








