Monday 22 February 2016

Kikosi cha polisi cha wanamaji Tanzania kimekamata Jahazi likiwa limesheheni bidhaa tofauti na zinazoonyeshwa na kibali.




Kikosi cha Polisi cha wanamaji kimekamata jahazi likiwa linatokea bandari ya Zanzibar kwenda bandari ya Dar es Salaam likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo spika za redio na friji wakati jahazi hilo liliondoka bandari ya Zazibar kibali chake kikionyesha kuwa limebeba mafuta ya marashi.
 
ITV ilifika makao makuu ya kikosi hicho na kukuta jahazi hilo linaloitwa Najat likiwa limejaa vifaa hivyo huku polisi na wafanyakazi wa jahazi hilo wakisaidia kushushwa kwa vifaa hivyo ambapo kamanda wa kikosi hicho Semboje Kanga amesema nyaraka za mzigo haziendani na kilichobebwa.
 
Katika hatua nyingine wenye mzigo huo wamejitokeza na kusema kuwa wananyaraka zote muhimu na wanashindwa kuelewa kwa nini polisi wanasema shehena hiyo wanamashaka nayo.
 
Naye mliki wa chombo hicho kilichokamatwa Bw Iddy Hadibu amesema kilichotokea ni kwamba wakati wanakuja bandari ya Dar es Salaam baharini wakakuta chombo kingine kimelemewa na mzigo na ndio wakawasaidia ili wasipate shida na hapo ndipo walipojikuta wanaingia katika dhahama hiyo.


Chanzo: ITV Tanzania

No comments: