Monday 22 February 2016

Mabibi na mabwana hapa nimewawekea taarifa kamili kuhusu Waziri Kairuki kutumbua majipu


Mawaziri wa Magufuli wameendelea kumiliki vichwa vya habari  kutawala katika Wizara mbalimbali Tanzania ambapo leo imegusa katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ambapo Waziri wake Angellah Kairuki ametangaza kuwaondoa kazini watumishi watatu kwa ubadhirifu wa mali za Umma.
Amesema ‘namsimamisha kazi Said Nassoro aliyekua mkuu wa chuo cha utumishi wa Umma kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake na kushindwa huko kusimamia kikamilifu, kumepelekea shughuli za matawi ya chuo hiki mikoani kuathirika na kutoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhirifu wa mali za umma’
‘Kuanzia mwaka 2011 mpaka 2013 mkuu wa chuo tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la gorofa mbili katika tawi letu la chuo huko Mtwara, CAG na TAKUKURU walithibitisha ubadhirifu huu lakini mkuu huyu wa chuo niliyemsimamisha hakuchukua hatua na badala yake alimuhamishia Ngata Tabora na kuendelea na wadhifa wake’
Waziri Kairuki ameeleza pia ‘Ngata naye anasimamishwa kazi, na wa tatu ni Mbwilo Joseph ambaye mwaka 2013 alitumia vibaya pesa za malipo ya ada Bilioni moja zilizolipwa na Wanafunzi ambapo pamoja na ubadhirifu huo kugundulika bado mkuu wa chuo Nassoro alimteua kuwa kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa utawala na fedha, naye kuanzia leo anasimamishwa’

No comments: