Tuesday 23 February 2016

Simu yamfanya bodaoda kulivaa Lori, Inasikitisha sana hii imetokea Moshi


Tabia ya kudharau sheria za usalama barabarani imegharimu maisha ya mwendesha bodaboda, baada ya kulivaa kwa mbele lori aina ya Scania, alipokuwa akiongea kwenye simu huku akiendesha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 jioni, katika barabara ya Arusha- Moshi.
Kamanda Mungi alimtaja marehemu ni Joseph Asenga(30) mkazi wa Bonite na alisema mtu huyo aliyekuwa akiendesha pikipiki alikuwa akitokea Bonite alilivaa lori, wakati akijaribu kuhama upande wake huku dereva wa lori naye akijaribu kuhama upande wake ndipo walipogongana.
“Katika tukio hilo inaonekana kuwa dereva wa pikipiki na dereva wa lori wote waliokuwa wanakwepa, yaani kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yao ndipo walipokutana uso kwa uso hivyo kupeleka huyu dereva wa pikipiki kuingia chini ya lori na kugongwa,” alisema Mungi.
Alisema kuwa baada ya ajali hiyo dereva wa pikipiki alifariki dunia muda mchache, kabla ya kupewa matibabu katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.
Mashuhuda wa ajali hiyo Hamisi Mussa na Vicky Kimario, walisema kuwa dereva wa bodaboda alikuwa akizungumza na simu yake ya mkononi bila kutarajia kitakachotokea. “Hawa bodaboda ni wazembe sana, huyu kaka alikua anachati tangu nilipomuona mbele yangu, hakuwa na akili ya kuwaza kilichopo mbele yake akaingia chini ya lile lori na kupoteza maisha hapo hapo,” alisema Hamisi Mussa.
Vicky Kimario mkazi wa Moshi alisema wakati akivuka barabara alishuhudia bodaboda ikiingia chini ya lori na hatimaye aliyekuwa akiendesha hakutoka alikuwa ameshafariki dunia. “Simu ilimponza yule jamaa, alishindwa kujisaidia wakati wa tukio kwakuwa alinogewa na maongezi ya simu aliyokuwa akiwasiliana nayo, bila kujua wakati navuka barabara nilistaajabu kuona ameshakuwa maiti,” alisema Kimario.

No comments: