Monday 28 March 2016

Vanessa Mdee: Ninapovaa Nguo Fupi nina malengo haya


Muimbaji huyo ambaye ameachia video ya wimbo Niroge hivi karibuni, amekiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV kuwa, anapenda
kuvaa nguo fupi ili kutangaza brand yake, na hatimaye impe dili la matangazo kwa wabunifu wa mavazi.

Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past, wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao” alisema Vanessa

Aliongeza,”Mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili napigiwa simu na Balmain, na Louis Vuitton, nataka designers wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu kubwa na zinaendana, so nina malengo , na if I’m gonna offend anybody I’m sorry.”

Chanzo: Bongo5

Familia ya Rapper huyu yafikisha watoto Saba.


Rapper T.I. hataki mchezo.. Yeye na mke wake,Tiny wamepata mtoto wao wa saba.

Mtoto huyo wa kike alizaliwa wiki iliyopita. Taarifa hiyo ilitolewa na mtoto wa dada yake na T.I., Kamaya Harris.

My little cousin is here. Last night I went to go see my auntie and she had the baby today,” alisema kwenye Snapchat.

Watoto wengine wa familia ya Rapper huyo ni Messiah, Domani, Deyjah,King, Major na Zonnique.

Sunday 27 March 2016

Taarifa ya Chad kujiondoa #2017AFCON na Majibu wa mustakabali wa timu zilizosalia.


Taarifa za  timu ya Taifa ya Chad kujitoa kwenye mashindano ya AFCON zimekuja saa chache kabla ya kuvaana na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Mfano wa barua iliyobainisha Chad Kujitoa katika michuano ya #AFCON2017 (Picha na YerickoNyerere)


Baada ya kujitoa kwa timu hiyo sasa zitatumika kanuni za michuano hiyo zinazosimamiwa na CAF. Na huu ndio ufafanuzi wa hatma wa timu zilizopo kwenye kundi moja na Chad.

Kwa mujibu wa Kanuni sasa Matokeo yote ya Chad yamefutwa na hayatahusishwa na timu yoyote hata kama timu hiyo iliwahi kuifunga Chad na kujinyakulia pointi au kuwa katika nafasi iliyopo kutokana na magoli iliyoifunga Chad.

Kadhalika kundi litatoa mshindi mmoja ambae anashika nafasi ya juu zaidi kwenye kundi tofauti na makundi mengine yatatoa timu mbili za juu katika kundi.

Tweet kadhaa za CAF wakilitolea ufafanu sakata hilo la kujitoa kwa timu ya  Chad


Ikumbukwe Chad ilikuwa katika kundi G na Nigeria, Misri (Egypt) na Tanzania, Taifa Stars.

Siri ya maisha ya wasanii waliopo kwenye Lebo ya WCB. Harmonise Amefunguka.



Msanii kutoka lebo ya WCB Harmonize, ametoa siri ya maisha ya wasanii ambao wako chini ya lebo hiyo, ambayo inawafanya kuepuka mambo mengi ikiwemo skendo chafu, huku akidai kuwa wanafuata nyayo za bosi wao Diamond Platnums.

Harmonize ameongea hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kuwa wao kama WCB hawana kawaida ya kwenda club kutokana na kubanwa na majukumu, na pia hata bosi wao ambao ni mfano mzuri kwao, hana kawaida ya kwenda sehemu kama hizo.

“Labda nizungumze kitu kimoja, WCB sio mimi tu hata wasanii wengine ambao watatoka WCB kuna life style ambayo watafuata, lakini mimi kama mimi sipajui club kabisa, sijawahi kwenda club sitokagi, kwa sababu pale ofisini kuna studio studio mle mle ndani, kuna vyumba ambavyo ukirekodi ukichoka unakaa unarefresh mind, kuna game station mnakaa mnacheza game, alafu pia kuna vyumba vya kuishi mule mule, muda wenyewe wa kutoka unakosa, alafu pia ukizingatia CEO mwenyewe wa WCB hana hizo mambo za kwenda club, so sisi tunajifunza kupitia yeye”, alisema Harmonize.

Pia Harmonize amekiri kuwa umaarufu alionao sasa ndio unamfanya ashindwe kwenda sehemu mbali mbali pamoja na kujichanganya na wasanii wengine, kutokana na kutozoea mazingira hayo, huku akitamani maisha aliyokuwa nayo kabla, lakini pia kuna muepusha na skendo mbaya.

Juzi kulikuwa na mwaliko Mh Rais alialika wasanii Ikulu, mi sikuenda kwa sababu sijazoea hayo mazingira, kwa hiyo inakuwa ngumu kuhusishwa na skendo huyo mwanamke nakutana nae wapi, sababu muda wa kutoka nakuwa sina, mi sikutanagi na wasanii wenzangu yani, muda naukosa kabisa, na ndo kati ya vitu ambavyo navimisi kabisa”, alisema Harmonize.


Chanzo: UdakuSpecially

Friday 25 March 2016

New Video: SamMisago - Ballin and Bulling (Video Out now)



SamMisago Mtangazaji wa EATV ambae pia kwa siku za hivi majuzi ameamua kutuonyesha kipaji chake kingine tofauti na utangazaji alipozama katika tasnia ya Music Leo ametoka na Video mpya kabisa.

BongoHomeTz inakupa fursa ya kuitazama video hiyo inayokwenda kwa jina la Ballin and Chillin. Keep Watching.


New Video: Yemi Alade - Ferrari Official Video


Watch New official video from Nigerian Musician Yemi Alade- Ferrari.


Thursday 24 March 2016

Ukweli kuhusu Taarifa ya kucheleweshwa kwa Mishahara kisa uhakiki wa watumishi hewa


Kumekuwa na Taarifa zinazoeleza kucheleweshwa kwa mishahara kwa wafanyakazi mbalimbali kwa kisingizio cha utekelezaji wa Agizo la Mh. Rais John Pombe Magufuli alilolitoa alipokuwa akiapisha wakuu wapya wa mikoa ikulu mnamo March 15, mwaka huu.

Leo march 24 Ofisi ya Raisi manejimenti ya utumishi wa Umma imelitolea ufafanuzi suala hilo na hii hapa ni Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari.


New Video: Vanessa Mdee - Niroge Official Video



Saa chache baada ya Msanii Vanessa mdee kuachia audio Niroge DOWNLOAD AUDIO HAPA Ameachia video yake. Unaweza kuitazama Vanessa Mdee- Niroge Official Video



Audio | Ruby Ft. Wakazi - Sijutii REMIX | Mp3 Download



                      DOWNLOAD HERE

New Audio: Vanessa Mdee - Niroge



                         DOWNLOAD HERE

Wednesday 23 March 2016

Madee ashauri Serikali na Watumia Madawa nini kifanyike kutokomeza biashara


Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee Ali amesema kama angekuwa anatumia Madawa ya kulevya na tayari ameshaathirika basi angewataja wale wanaomuuzia ili kuisaidia serikali kutokomeza matumizi ya madawa ya kulevya.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Madee amesema serikali inaweza kutokomeza biashara ya Madawa ya kulevya kama ikiwatumia wale walioathirika.

Ningekuwa mimi natumia Madawa ya kulevya na tayari yameshaanza kuniathiri si utaulizwa imekuwaje kuwaje, nani amekufundisha hizi mambo, umeanza wapi umenunua kwa nani, ina maana nitaanza kumtaja yule ambaye ameniuzia, na ambaye ameniuzia mimi kikete, yeye atamtaja bosi wake, bosi wake atamtaja yule bosi wake mkubwa kwa hiyo ile cheni yote itakuja mpaka itamfikia yule kigogo anayeingiza kutoka nje”, alisema Madee

Pia Madee alisema ingawa wasanii wana nafasi yao katika kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya, lakini serikali ndio chombo ambacho kinaweza kupambana na biashara hiyo na inatokomeza kabisa.

Sunday 20 March 2016

New Video: Tazama Official Video kutoka kwa Amini- Hawajui


Tazama video mpya ya Amini-Hawajui.iliongozwa na Kwetu studios.


            

NEW SONG: Download Lady Jaydee- Ndi Ndi Ndi.… Ni Mpya kabisa


                         DOWNLOAD HERE

Ncha Kali amewaamulia wasanii, Asema kazi ndio mpango

Mtangazaji Reuben Ndege A.K.A Ncha Kali.
Mtangazaji Nguli nchini Tanzania ambae amewahi kufanya kazi zake katika vituo vya utangazaji vya Clouds Fm na baadae kuripotiwa kuamia E Fm Reuben Ndege (Ncha Kali) leo jumapili March 20,2016 ameitumia account yake ya Twitter kuongea na wasanii.

Ncha kali ametumia Tweets hizi Saba  zikiwa na kichwa kinachosomeka "Dear Wasanii" akiambatanisha na jumbe mbalimbali.









Saturday 19 March 2016

Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) baada ya kumalizika mechi za leo.



Siku ya Leo Jumamosi ya March 19, 2016 ligi kuu vodacom (VPL) ilikuwa na michezo mitatu ambapo  Coastal Union iliburuzana na Simba Sc, Stand United na Ndanda huku MajimajiFc ikicheza na Mbeya City.

Haya ndiyo matokeo baada ya mechi zote kumalizika
FT" Coastal Union 0 - 2 Simba SC
FT' Stand United 1 - 1 Ndanda FC
FT' Majimaji FC 3 - 1 Mbeya City

Baada ya matokeo ya mechi za leo huu ndio msimamo wa ligi.


Msanii Mwasiti Almas ameweka bayana mambo manne yanayomfanya avutie, Ugali na Dagaa vimo




Mwasiti akizungumza na EATV ametoa ya moyoni kuhusiana na mwonekano wake kwa sasa kuonekana anavutia zaidi tofauti na siku za nyuma.

''Kwa sasa nina mapenzi ambayo ni salama japo siwezi kumtaja Mpenzi wangu kwa sasa kwa sababu bado ni mapya ila nina faraja sana'' amesema Mwasiti

Pamoja na hayo Mwasiti amesema kwamba aina za vyakula kama ugali na dagaa na kupumzika sana hinachangia pia muonekano wake kuonekana wa kuvutia.

Ikumbukwe Mwasiti ni msanii wa kike mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni ambae amekamalia katika gemu ya muziki wa bongo. Pata futsa ya kuitazama video hii ya mwanadada Mwasiti.

Mwasiti ft Queen Darleen- Sema nae

Zitto Kabwe ateta na waziri wa mambo ya ndani kuhusu Kutoweka kwa mwandishi wa DW.

Mh. Zitto Kabwe 


Kiongozi mkuu wa Chama cha wazalendo ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini mh Zitto Zuberi kabwe ameiambia wizara ya mambo ya ndani ieleze alipo mwandishi wa habari wa DW kiswahili.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika "Waziri wa mambo ya ndani aeleze Mwandishi Salma Said yupo wapi? Kashikiliwa Kituo gani cha Polosina kwa kosa gani?"

Kivuli cha Teet ya mh Zitto Kabwe.
Kadhalika kuna taarifa ambazo BongoHomeTz haijazithibitisha, Zikiwa na kichwa kinachosema "Baraza la habari nchini Tanzania MCT kwa kushirikiana na taasisi nyingine nne zimetoa siku mbili kuanzia leo kwa jeshi la polisi nchini kuhakikisha linafanya uchunguzi na kufanikiwa kumpata mwandishi wa habari Bi. Salma Said anayedaiwa kutekwa."


BOFYA KIUNGO HIKI KUISOMA.

Ommy Dimpozz: Mwaka huu nitamtambulisha msanii katika Lebo yangu ya PKP

Ommy Dimpozz kwa poz Tanzania Musician 
Muziki wa Tanzania unaelekea kukua zaidi kutokana na mastaa kibao kuanzisha lebo zao kuwasaidia wasanii wanaochipukia.

Akizungumza na kipindi cha Friday Night Live,kinachoruka kupitia EATV, Ommy Dimpoz alisema mwaka huu atamtambulisha msanii mmoja kutoka lebo ya PKP kwa kirefu Poz Kwa Poz

Baada ya kuanzisha lebo yangu ya PKP, Mwaka huu kumtambulisha msanii wangu mmoja. Najua watu watasema kuwa mpaka fulani aanzishe na wewe ndio uige,Ila nilitangaza muda kuwa nimeanzisha lebo yangu.” Alisema Dimpozz

Ommy Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha Achia Body ambacho kwa sasa kina walau takribani miezi mitatu ivi.




Friday 18 March 2016

Interview: Msanii Chemical aeleza mahusiano yake na kiongozi wa Kazi kwanza records.

Claudia Benezeth Lubao aka Chemical (Picha na maktaba)

Hit maker wa ngoma ya ‘Sielewi’ Claudia Benezeth Lubao aka Chemical alianza ku rap tangu akiwa anasoma sekondari “Twiga Secondary School”, Kisha akahitimu degree yake ya ‘Fine and Performing Arts’.

Kwa sasa Chemical yupo chini ya label ya ‘Kazi Kwanza Records’ na ameshafanya kazi kadha ‘Sielewi’, ‘VIP’ na ‘Party’ kupitia mikono ya producer Maxmaizer.

BongoHomeTz imenasa sauti ya Chemical alipokuwa akizungumza na      The Cruzz Friday Bang ya ArushaOne Fm (101.6MHZ)

Amezungumzia jinsi alivyoingia katika  lebo ya Kazi kwanza records,Mipango yake ili aweze kudumu kwenye game ya Music na Colabo alizofaya Na wasanii wakubwa wa Hip Hop hapa Tz

       MSIKILIZE CHEMICAL HAPA

Thursday 17 March 2016

New Video: Vicelah ft J Deal - Miss Sanawari


Tazama video mpya kutoka kwa msanii anaetokea mkoani Arusha Vicelah ft J Deal - Miss Sanawari.



Mo Town: Kukosa meneja kunaugharimu muziki wangu.

Msanii Chipkizi kutokea mkoani Kilimanjaro Mo Town Star (Picha na Maktaba)


Msanii Mo Town Star anayewakilisha vyema Mkoa wa Kilimanjaro amesema kwa sasa yupo studio akiandaa wimbo mpya.

Mo Town Star ameiambia BongoHomeTz kuwa kwa sasa anajipanga kutoa wimbo mpya ambao amesema anaamini mashabiki wake watapata ladha tofauti na waliyoizoea.

"Ni International song, ninafanya Na producer mkubwa Na pia Ni studio kubwa hivyo nategemea utakuwa wimbo mkubwa pia" alisema Mo Town Star.

Hata hivyo Mo Town Star ameongeza kwa kwa kueleza kuwa anachelewa kufanya kile anachofikiria kukifanya kutokana Na kujisimamia mwenyewe kwani hadi sasa hivi Hana meneja.

"Sina meneja, najisimamia mwenyewe Na nimeweza kupiga hatua kubwa, nahisi nikipata meneja nitafika ninapotaka kwa kuwa najiamini Na ninatambua ninachofanya" ni maneno ya Mo Town Star alipozungumza nasi.

Mo Town Kwa sasa anafanya vyema Na wimbo wake wa "Nikuache Uende" ambao umepokelewa vizuri Na Mashariki wake lakini pia anafanya vizuri Na nyingine kama Mapenzi Na wewe, Mapenzi Kamari Na nyinginezo.

Unaweza kudownload moja ya nyimbo za Mo Town star kwa kubofya HAPA KUDOWNLOAD Mo Town Star-Nikuache uende.

Wednesday 16 March 2016

Mtoto Mchanga aibiwa Wodini katika hospitali ya Mkoa wa Arusha


Hali ya sintofahamu imeibuka katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru baada ya mtoto mchanga wa siku tano kuibiwa wodini katika mazingira ya kutatanisha.

Tukio hilo limezusha hofu kwa baadhi ya wazazi waliojifungua katika wodi ya wazazi hospitalini hapo wakihofia usalama wa watoto wao na kuomba Serikali kuingilia kati.

Akisimulia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Sinyari Lucas ambaye ni mkazi wa Simanjiro mkoani Manyara, amesema limetokea usiku wakuamkia jana.

Akizungumza huku akiwa ameghubikwa na huzuni, Bi Sinyari
amesema wakati akiwa kitandani muda wote kabla ya kulala alikuwa na mtoto wake.

Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Jackline Urio amekiri kuwapo kwa tukio hilo na kwamba, uongozi umelipokea kwa mshtuko mkubwa na unalifanyia kazi.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amesema wamepokea taarifa hizo na tayari ameagiza maofisa kwenda kufuatilia tukio hilo kwa kina.

Tuesday 15 March 2016

Tayari imethibitishwa mkuu wa wilaya ya Arusha kutapeliwa milioni 10 Mtandaoni


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00 usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.

Mkuu huyo wa Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.

Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.

Wizi wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo

Audio: Exclusive Interview Na Best Nasso



Msanii wa Bongo Best Nasso anaetamba na nyimbo yake ya  ya Rumba amefunguka mambo kadhaa kuhusu muziki wake ikiwemo sababu za nyimbo zake kutokufanya vizuri.

Best Nasso ameiambia BongoHome Tz kuwa moja ya sababu kutokufanya vizuri ni kutokana na kuziwahisha sana.

Kadhalika amezungumzia hatua yake ya kufanya video nje na ni msanii gani anatamani kufanya nae kolabo.

      SIKILIZA FULL INTERVIEW HAPA

Audio: Download wimbo mpya wa Nashapai Ft Linex-Angejua


Baada ya Harmonize kuingia Wasafi na kufanya vizuri kichwa kingine kinakuja


Lebel ya Diamond Platnumz ‘Wasafi’ imetangaza rasmi kumtambulisha msanii mpya baada ya mafanikio makubwa ya Harmonize.

Kupitia twitter na Instagram Diamond Platnumz ametufahamisha haya.

Monday 14 March 2016

ZEC: Karatasi za uchaguzi wa marudio zitaingia Zanzibar Tar 17 Mwezi huu

Karatasi za kupigia kura kwa ajili ya 'Uchaguzi
Mkuu wa Marudio', Zanzibar, uliopangwa
kufanyika siku ya jumapili, tarehe 20 Machi
mwaka huu, sasa zitawasili visiwani Zanzibar siku
ya Alhamis, tarehe 17, Machi 2016.

Barua ya ZEC kwa vyombo vya habari. (Picha na Ally Mohamed-Zanzibar)

Kandoro: Umri unaruhusu kumshawishi Raisi kuniacha Ukuu wa mkoa

Abas Kandoro (Picha na Maktaba)
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli  alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro.

Kipindi cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro asubuhi ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari amefikia kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea kutumikia nyadhifa hiyo.

“Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono katika nafasi hii.

“Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro.

Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya

Sunday 13 March 2016

Download | Bonta Maarifa Ft Nikki Wa Pili Belle 9 - Usirudi Jela [Audio]

   

                    Download Here

List nzima ya wakuu wapya wa mikoa. Kama ilivyotoka ikulu Leo



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliamefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 March, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo
  1. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zelote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14. Jordan Mungire Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16. Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara.
  17. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18. John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19. Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21. Joel Nkaya Bendera – Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23. Rehema Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24. Mhandisi Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa – Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Gerson Msigwa, wakuu wote wa mikoa walioteuliwa wataapishwa Jumanne tarehe 15 March 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Dar es salaam.

Katibu NACTE amejiuzulu nafasi yake.

Katibu Mtendaji wa NACTE (Aliyejiuzulu) Dokta Primus D Nkwera (kulia) akifafanua jambo


Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.


Uamuzi wa kujiuzulu kwa Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi kuu za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Dar es Salaam juzi na Mwenyekiti wa Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kuangua kilio.


Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu ili kulinda hadhi ya Nacte kutokana na habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.


Gazeti hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405 lilimtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera kughushi vyeti vya shahada ya uzamivu baada ya kusomeshwa na serikali Afrika Kusini na kufeli.


Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi kushikwa na mtu mwenye tuhuma ya aina yoyote, na ametafakari na kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa pembeni.


"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja ya Dr. Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:


"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.


"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa, yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana na ukatibu utendaji.


"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati mwingine lazima mkubaliane na hali hii, lakini pia endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama kawaida kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."


Kutokana na kujiuzulu kwake, Mlote alisema bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu nyingine zikiendelea.


Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini akaahidi kuendeleza yote aliyoyaacha.

Saturday 12 March 2016

Nick Minaj na Meek Mill bado ni wapenzi

nickiminajmeekmill
Nicki Minaj na Meek Mill wametumia mtandao wa snapchat  kukanusha kuwa wameachana.

meek-mill-nicki-minaj-snapchat

Picha hii ni miongoni mwa picha zilizosamba mtandaoni zinamuonyesha Nicki Minaj akiwa na Meek Mill kwenye pozi flani la kimahaba.

Mwezi uliopita Meek Mill na Nicki Minaj waliripotiwa kuachana sababu ya kifungo cha ndani cha Meek Mill kinachomuweka nyumbani kwake Philadelphia.