Tuesday 3 May 2016

Mtangazaji wa Clouds amtaja Adam mchomvu akilaumu Redio nyingine.


Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema
nyimbo zake pamoja na za mtangazaji
mwenzake, Adam Mchomvu zinabaniwa na redio yingine, kitu ambacho anaona si sawa.

Amesema redio za mikoani ndizo zimekuwa
zikiwapa support bila kujali kuwa wanatoka
Clouds lakini redio karibu zote za Dar zimekuwa zikibania nyimbo zao.

Diva ambaye anaandaa album yake, The Life of The Diva, amesema kuwa hicho ni kitu ambacho angependa kuona kinafutika.

Mimi naona wako so unprofessional, mbona sisi Clouds FM watu wazuri, Sam Misago kaja, katoa wimbo ataitwa kwenye XXL nyimbo yake itachezwa, sisi mbona nyimbo zetu hamchezi?” amehoji Diva.

Diva anaendelea kusema “Nilipeleka nyimbo East Africa Radio na ina haki zote za kuchezwa na haikuchezwa kwasababu natoka Clouds Media, kwanini wanatufanyia hivi? Hii ni biashara, wao wafanye kazi zao, na sisi tufanye kazi zetu lakini when it comes to music, sisi tunafanya serious kabisa"

Chanzo: Bongo5

UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NA MINYORORO YA VIKWAZO!



Na Ally Mohammed Abdul-rahman,
Zanzibar, Tanzania,
Simu: + 255 655 572 594,
Barua-pepe, allymohammed01gmail.com

Leo, Jumanne, tarehe 03 Mei, ni Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani, kwa muktadha wa neno "UHURU" linalenga kutoa nafasi, kutokuingiliwa, kutokupangiwa, kutokubugudhiwa na kila aina ya kuachwa kujiendesha ufanye kazi yako bila ya bugudha kutoka kwa mamlaka yeyote ilimradi sheria za nchi zinafuatwa.

Wakati tunasherehekea siku hii muhimu kwa taaluma yetu ni wazi kuwa tuna safari ndefu sana huko mbele, Uhuru wa Vyombo vya Habari 'umebakwa' na 'kunajisiwa' hadharani na wanasiasa, mamlaka za serikali, wamiliki wa vyombo vya habari, matajiri na hata baadhi ya taasisi zenyewe za habari.

Ndiyo! Umebakwa na kunajisiwa, tunahubiri kwenye vinywa na maandishi tu juu ya Uhuru wa Vyombo vya Habari lakini hatutendi vile tunavyohubiri katika vinywa vyetu.

Ni utamaduni wa kawaida kila ifikapo siku kama hii, wadau wa sekta ya habari nchini wakiongozwa na magwiji na wakongwe wenye uzoefu wa kushiba katika tasnia hii kukutana na kuangalia changamoto za tasnia na namna ya kuzishughulikia.

Mwaka huu Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanaadhimishwa kitaifa jijini Mwanza huku yakibebwa na kauli mbiu ya “KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI, IDAI".

Maadhimisho haya yanafanyika kitaifa kwa mara ya nne na yanalenga kukumbusha umma na dunia kwa ujumla umuhimu wa vyombo vya habari, kufanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu ama chombo chochote.

Zaidi ya wadau 250 wakihusisha waandishi wa habari wakongwe na wanaochipukia, wahariri, viongozi wa mashirika wahisani wa ndani na nje, wawakilishi wa mihimili ya nchi (Serikali, Bunge na Mahakama), wasomi wa vyuo vikuu na mabalozi mbalimbali wamekusanyika jijini Mwanza kwa ajili ya maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni leo.

Ni hatua nzuri na kweli kuna baadhi ya mabadiliko yanaonekana kutokea kutokana na mikutano ya aina hiyo, lakini niseme bado changamoto zipo nyingi sana katika kupata uhuru wa vyombo vya habari kivitendo na sio porojo zisizokuwa na tija yeyote.

Yapo matukio kadhaa ambayo yanafanyika bila ya kificho kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari, matukio hayo yanafanywa na makundi niliyoyataja hapo juu.

Ni dhambi kitaaluma kwa mtu ambaye hana hata introduction (utangulizi) ya uandishi wa habari halafu eti anatoa maelekezo news room (chumba cha habari) habari gani iende na habari gani isiende kwa interests (matakwa) binafsi ambazo kimsingi zinaingilia uhuru wa habari.

• Kuna baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wamechukuwa jukumu la kuwa wahariri kwenye 'media house' wakati hawana taaluma yeyote ya habari, hiki ni kiwango cha uzamivu (PhD) cha dharau.

• Wapo baadhi ya wanasiasa wamefanikiwa kupenya ndani ya vyombo vya habari na kuvimiliki kitaaluma wakati wenyewe hawana elimu yeyote inayohusu habari.

• Wapo matajiri wanaotumia fedha zao kulazimisha habari wanazozitaka wao, kama kuna habari za 'kuwabomoa' hata kama zipo kimaadili watatumia nguvu ya fedha zao kuizima habari hiyo kwa gharama yeyote.

• Zipo baadhi ya mamlaka za serikali ambazo kwa asilimia kubwa wao ni maadui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari, hawataki hata kusikia hizo habari zinazohusu uhuru wa habari, ukiikosoa serikali hata pale ambapo unalazimika ukemee kwa misingi ile ile ya taaluma na utawala bora kama wanavyohubiri basi utageuka adui usie na kikomo na watakushughulikia kwa njia zote za haramu wanazozijua wao.

• Kuna hizi taasisi za habari mfano wa MCT na TEF, baadhi yao, narudi baadhi yao na sio miongoni mwa huo mfano wangu, zenyewe zimegeuka kuwa upande wa serikali hata pale zinapoona Uhuru wa Vyombo vya Habari 'unanyongwa', watakaa kimya kama hawapo, hata 'press releases' zitawashinda kisa, wapo chini ya 'kwapa' za serikali na wao wanalinda 'mkate' wa kila siku (unafiki uliopitiliza).

Changamoto ni nyingi na haziwezi kutatulika kirahisi kama hatujaunganisha nguvu na kuwa na sauti moja ya kuisimamia taaluma na kuacha 'kuabudu' wanasiasa na taasisi za serikali zinazotumia nguvu kubwa kuminya na kunyamazisha kabisa kitu kinachoitwa "Uhuru wa Vyombo vya Habari".



Ukiwasikiliza na matendo yao ni vitu vinavyokinzana, ndiyo msingi wa kusema wanayoyaandika na kuyatamka ni tofauti sana na matendo yao, kiufupi hawana nia njema na wala hawapo tayari kuona uhuru wa vyombo vya habari unapatikana.

Pengine kwa kuwa serikali na wao wanamiliki vyombo vya habari na kimsingi vyombo hivyo haviwezi kutoka nje ya sera za serikali na wakati mwengine baadhi yao vinatumika kueneza 'propaganda' pale ambapo
wangepaswa kuikosoa serikali na kuwaonesha njia sahihi ya kupita, lakini watapata wapi nguvu hiyo wakati wapo chini ya usimamizi wa serikali?.

Ingawa kimsingi vyombo hivi vinatakiwa viwe vya umma na sio kuwa upande wa serikali hata kwa machafu lakini ni kama tayari 'vimetekwa' na sio tu kuwa upande wa Serikali bali kuwa sehemu ya propaganda na kuwa wasaidizi wa chama tawala kwenye kampeni za uchaguzi.

Ni tofauti na mashirika ya umma ya habari ya mataifa mengine kama vile Afrika ya Kusini (SABC) au Uingereza (BBC) ambapo wao vyombo hivi vinahudumia umma na sio kuwa wasemaji wa serikali na kusifia kila kitu cha serikali huku wakitetea hata yasiyostahili kutetewa.

Changamoto za waandishi wa habari sitozigusa hapa maana nalo ni JIPU lililopiga rangi, nitatafuta nafasi nyengine kulitumbua hili.

Tuadhimishe Siku ya Uhuru wa Vyombo wa Habari tukijua tuna dhima ya kuyatekeleza kwa vitendo yale tunayoazimia katika vikao vyetu vya tathmini ya tasnia hii.

Haitoshi kuadhimisha kwa kula, kunywa, kupeana posho kubwa na kupiga picha nyingi za pamoja na mgeni rasmi kisha yale ambayo yanakwamishwa kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari tukayapuuza na kuja kujikumbusha tena kwenye maadhimisho mengine mwakani.

Vyombo vya Habari vina nguvu kubwa kama tutashikamana kwa umoja wetu na nguvu ya kalamu zetu heshima yetu lazima itakuja kwa kiwango kinachokubalika, kinyume chake tutaendelea kudai uhuru wa vyombo vya habari kila siku na milele hatutaona mabadiliko kwa hili.

Monday 2 May 2016

New Song: Huu ni wimbo mpya ya Harmonize ft Raymond - Penzi.


Wasanii kutoka Lebo ya Wasafi Classic, Harmonize na Raymond wameimba kwa pamoja huu wimbo unaitwa “Penzi”. Wimbo huu haujatoka rasmi.

Meneja ambaye anawasimamia wasanii hao, Ricardo Momo amesema wimbo huo umetoka bahati mbaya tu ulikuwa kwenye flash wakati wapo Mwanza kwenye show walisahau hiyo flash.

DOWNLOAD HERE

Thursday 28 April 2016

Majengo 20 ya CCM Kubomolewa Moshi.


Ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kinyume na sheria za mipango miji katika Manispaa ya Moshi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Ubomoaji huo unakusudiwa kuambatana
na uvunjaji wa majengo zaidi ya 20 ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyopo katika Kata ya Mawenzi.

Meya wa manispaa hiyo, Raymond Mboya
amewaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kusimamia ipasavyo sheria hiyo ili kuhakikisha majengo yaliyojengwa kinyume na sheria yanavunjwa.

Mboya amesema sheria ni lazima ifuatwe
haijalishi ni chama gani kimejenga kinyume.

Leo tunapata ugumu wa kuwa jiji kutokana na sisi wenyewe kushindwa kusimamia sheria za mipango miji, hatuwatendei haki wakazi wa Manispaa ya Moshi ni lazima ifike wakati watu
tujue kuna mamlaka ambayo imekabidhiwa kusimamia mji,”amesema Mboya.

Kwa upande wake Loth Ole Mesele, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini amesema hajapata taarifa hizo za kubomolewa kwa majengo ya chama hicho.

Magufuli amsimamisha kazi kisa hachukui mshahara.


Rais Magufuli ametengua uteuzi wa
Mkurugenzi Mtendaji TIC, Bi Juliet Kaoruki ambapo pamoja na mambo mengine sababu ya Mh Rais. Kutengua uteuzi huo ni kutokana na kutochukua mshahara wa serikali.

Kadhalika Bi. Kairuki ameingia kwenye list ya watumishi kadhaa wa serikali waliosimamishwa kazi na kupewa ahadi ya kupangiwa kazi nyingine.

Kivuli cha taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo  April,28 2016


Wednesday 27 April 2016

Uhaba wa umeme wasababisha watumishi wa umma kufanya kazi siku kwa wiki Venezuela.



Serikali ya Venezuela imeagiza wafanyakazi
wake wawe wakifanya kazi siku mbili kwa wiki.Hii ni hatua ya muda iliyochukuliwa kutokana na uhaba wa umeme.

Makamu wa Rais Aristobulo Isturiz ametangaza kwamba watumishi wa umma wanafaa kufika kazini Jumatatu na Jumanne pekee hadi mzozo wa sasa wa nishati umalizike.

Venezuela imekabiliwa na ukame mkubwa ambao umepunguza maji kwenye bwawa lake kuu la kufulia umeme.



Lakini upinzani umeituhumu serikali kwa
kutodhibiti vyema mzozo wa sasa. Agizo la kupunguzwa kwa siku za kufanya kazi,
lililotolewa kupitia runinga ya taifa na Bw Isturiz.

"Hakutafanywa kazi katika sekta ya umma
Jumatano, Alhamisi na Ijumaa, ila tu majukumu muhimu sana.” alisema.

Amesema Venezuela imeathiriwa sana na hali ya hewa ya El Nino na kwamba hali ya kawaida itarejea baada ya mvua kuanza kunyesha.

Serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa
kupunguza matumizi ya umeme. Februari, maduka yaliagizwa kupunguza muda
ambao yanafunguliwa kila siku na pia kujaribu kujizalishia umeme.

Mapema wiki hii, serikali pia ilisongeza mbele saa kwa nusu saa ili kupunguza mahitaji ya umeme kwa ajili ya mwanga mapema jioni.

New Song: Barnaba - Wanifaa.(MP3)



DOWNLOAD HERE

Tuesday 26 April 2016

New audio: Nuh Mziwanda Ft Ally Kiba - Chupa Jike



                  DOWNLOAD HERE

Mke Wa rais mstaafu wa Kenya afariki dunia Jumanne hii


FirstLady wa zamani wa Kenya Lucy Kibaki amefariki dunia Leo Jumanne.

Taarifa ya Rais Uhuru Kenyatta imedai kuwa Mrs Kibaki alifariki akitibiwa katika hospitali ya Bupa Cromwell ya London.

“Her excellency has been unwell for the last one month and has been receiving treatment here in Kenya and subsequently in the United Kingdom,” yamesema maelezo hayo.

Mrs Kibaki alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Nairobi mwezi uliopita baada ya kutafuta matibabu katika hospitali ya Gertrude ya Muthaiga.

Ameacha watoto wanne, Judy Wanjiku, Jimmy Kibaki, David Kagai na Tony Githinji.

Watatu wakamatwa wakisafirisha Madawa Kilimanjaro


Watu watatu akiwemo mmoja raia wa Kenya
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa
ya kulevya aina ya Mirungi na Bangi kilo 54
na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa
kutoka nchini Kenya kwenda mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro
Bw.Wilbrod Mutafungwa amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa katika
maeneo ya njia panda Himo wilaya ya Moshi
na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye
miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi
miguuni.

Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor
mfanyabiashara mkoani Arusha, Naftal Mvoyi
mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis
mkazi wa Arusha ambao walikuwa
wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia
magazeti na gundi ya karatasi na kisha
kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa
wakitokea nchini Kenya kuelekea jiji la
Arusha.

Ripota wetu amefanikiwa kuzungumza na
baadhi ya vijana wanaojihusisha na matumizi
ya madawa ya kulevya katika manispaa ya
Moshi na kueleza kwamba changamoto
kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali
inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na
matukio ya uhalifu.

Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri
vijana wengi kiafya kutokana na baadhi yao
kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na
hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya
wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

MJ record yavunja mzizi wa Fitna Video ya Sugu- Freedom


Mr Blue analalamika kuwa Sugu ameupora
wimbo wake ‘Freedom’ aliokuwa amemshirikisha kwa kutoa verse zake na kuufanyia video iliyotoka jana.

Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. MJ Records walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.

Producer mkuu wa studio hiyo, Marco Chali
ameuambia mtandao mmoja kuwa beat ya wimbo huo ilitengenezwa na mdogo wake, Daxo Chali aliyetengeneza chorus yake na alimpa msanii wake Lizzy aliyeingiza.

“Ngoma ilikuwa ipo tayari na ilikuwa inasubiria verse tu kadhaa halafu ilikuwa ni ngoma yake [Daxo]. Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa akasema atamshirikisha Mr Two,” amesema Marco.
Walipoifanya, Blue aliiamua kuiachia kupitia
Mkito peke yake kwa maana kwamba hakuiachia ngoma rasmi. Anasema baada ya muda Sugu alimpigia simu kumuomba kuwa afanye version nyingine ya wimbo huo na aifanyie kabisa na video.

Anadai alimuambia Sugu aongee na Daxo
waliyekubali kuufanya tena hadi video ikafanyika huku yeye [Marco] akiwa hajui chochote kilichoendelea baada ya hapo. Na Marco anasema pia hakuhusika kwenye uingizaji wa sauti zote mbili zaidi ya kuzifanyia mixing peke yake.

Marco amesema anadhani wawili hao [Sugu na Blue] waliongea kuhusu hatua hiyo na kwamba wao kama studio hawakuwa na kipingamizi chochote kuhusu kurudiwa kwa wimbo huo kwasababu walitaka wimbo ufike mahali.

Hata hivyo Marco amedai kuwa wote wawili [Sugu na Blue] hawakulipia wimbo huo na
kwamba MJ Records iliwapa kwasababu ya ‘love’ tu. Marco anasema anashangaa kuona Mr Blue sasa hivi anatoa malalamiko hayo.

“Ni kwasababu mimi nilipenda tu kutoa studio
bure kwanini usijitahidi ukapeleka hiyo nyimbo ikafika sehemu ikafahamika, at least pia akili za watu zilizotumika watu wazione. Na ndio hicho kitu naona ni kizuri, yeye kwa mfano angefanya hata video, sidhani kama Sugu angerudia huo wimbo,” ameongeza Marco.

“Na yeye aliposema kwamba anataka afanye
video, namaanisha kwamba walishaongea na
Blue kwamba yeye afanye video. Halafu Daxo
wasije kumweka tena kwenye matatizo
akaonekana kwamba ni producer mzinguaji ni
vitu ambavyo havitamsababishia biashara na dogo mwenyewe ndio anataka kutoka. Na anajua wazi kuwa ni watu wazima wameongea kule,” amesisitiza Marco.

Naye Sugu amedaiwa kujibu malalamiko ya Blue kwa ujumbe huo chini kwenye WhatsApp.

Chanzo: Bongo5

Sugu Ndani ya tuhuma za wizi wa wimbo.


Msanii Mr blue kupita account yake ya Instagram amelalama akieleza mashambulizi yake kwa mbunge Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu au Mister II baada ya Sugu kuachia video ya wimbo unaokwenda kama "Freedom"

Mr Blue ameandika alifanya wimbo huo na Sugu ila ameshangazwa na kitendo cha Mbunge huyo kuondoa Verse yake na kuingiza mengine mwenyewe bila kumpatia Taarifa.


BongoHomeTz imejaribu kumtafuta Joseph Mbilinyi kwa Simu yake ya mkononi bila mafanikio.

Mbunge Joseph Mbilinyi A.K.A Sugu ametoa video ya wimbo mpya. Sugu-Freedom (Official video)


Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) baada ya kimya kirefu katika kazi yake ya awali ya Music sasa ameachia Video ya wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la "Freedom".

Tazama video ya Sugu hapa.Imeongozwa na Hanscana


            

Wednesday 20 April 2016

Donald Trump na Hillary Clinton Watambiana kwa kura.


Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa katika
uchaguzi wa awali wa vyama katika
kinyang’anyoro cha urais nchini Marekani katika mji wa New york, zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi mkubwa zaidi.

Hillary Clinton ambaye amemshinda mpinzani
wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa
ameeleza katika hotuba yake kuwa ushindi wa
chama chake cha Democratic umeweza
kuwaunganisha zaidi wapinzani wake kuwa
wamoja.

Hata hivyo New York inatajwa kuwa ngome
nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye
hesabu za kura zake zimeonekana kugoma
mapema kabisa katika chama chake cha Republican.

Wakati Hillary Clinton amemshinda mpinzani
wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa,
amewaambia wapinzani wake kuwa kuna la
ziada linalowafanya wawe wamoja zaidi ya
kuwagawa.

Source: BBC NEWS

Mrembo Naj avikwa pete ya Ahadi na Barakah Da Prince




Barakah Da Prince ambaye kwa sasa amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa kike, Naj, amedai kupiga hatua zaidi kuelekea
kwenye uchumba.

Amefunguka kuhusu
uhusiano wao alipokuwa akizungumza na moja ya mitandao mikubwa nchini Tanzania uitwao Bongo5.


Yeah ni kweli mimi na Naj tuna uhusino na hadi kwetu nimeshamtambulisha na yeye kwao najulikana na pia nimemvisha pia pete, sio ya uchumba ila ni Promise Ring,” amesema
Barakah.

Kuhusu kufanya kazi Barakah amesema “kuna kazi pia ambazo tumefanya ila hazitatoka sasa hivi hadi kwanza kila mtu atoe single yake halafu ndio itakuja hiyo ngoma ya pamoja mimi na Naj,”



Naj Amethibitisha kwa kusema
"Ni kweli Barakah amenivisha pete kama
alivyosema. Kwangu ni furaha sana maana
nimeshakuwa na mahusiano yaliyopita lakini
sikuwahi kufanya kitu kama hiki. Naona kabisa kuwa mahusino haya ni ya ukweli na naona kuna malengo kabisa, nafurahia kwakweli.”

Na kuongeza “Bado hatujaanza kuishi wote ila muda mwingi tupo pamoja, nafurahia mahusiano yangu ya sasa"

Saturday 16 April 2016

T.I.D Amenyoosha Maelezo. Juma Nature asema Magufuli atosha.



Baada ya KR kujitambulisha kuwa yeye ndiye Rais wa RADA Entertainment na Juma Nature kumpinga kwa kejeli akisema hamtambui Rais yoyote zaidi ya Rais Magufuli hatimaye TID anyoosha maelezo.

T.I.D amesema muda ukifika watamuapisha rasmi KR Mulla kuwa Rais wa Radar Entertainment na kutoa sababu za kufanya kazi na KR Mulla katika label yake.

Zaidi eNews ilipotaka kupata maelezo ya kina juu ya tuhuma za TID kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, TID aligoma kusema chochote, na hata alipoulizwa juu ya tuhuma hizo kwa wasanii wengine pia TID alisema “Muda ukifika nitaongea nyie endeleeni kuongea vitu msivyovijua”.

Wednesday 13 April 2016

Olamide ameweka wazi kumkubali msanii huyu.


Boss wa YBNL , Olamide, Hakika amekuwa akitambua na kukubali kazi nzuri inayofanywa na yeyote akisikia na kuona kipaji na sasa amemkubali mwimbaji Simi.

Simi’s Ni msanii Chipkizi nchini Nigeria ambae amekuwa amefanikiwa kumkuna Olamide kwa audio na video zake nzuri anazozitoa.

 “Simi is too talented!.” aliema Olamide, ambapo tayari msanii Sami tayari ameshajiunga na lebo ya Oscar Music Production ambayo inasimamiwa na
producer na mwandishi wa mashairi mwenye kipaji, Oscar Heman Ackah.

Diamond Platnumz: Heri niwe na Kijiji cha Nyumba Tandale kuliko ninunue nyuma Marekani.


Msanii Diamond Platnumz amefunguka
kuhusu suala la yeye kutonunua nyumba nchini Marekani kama wasanii wenzake wakubwa wa Afrika wanavyofanya.

Diamonda amefunguka hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa haoni umuhimu wa yeye kununua nyumba Marekani, tofauti na alivyonunua Afrika Kusini, kwani kule ilimlazimu.

Pia Diamond aliweka wazi kuwa kununua nyumba Marekani kwake hakuna faida, ni heri awe na kijiji cha nyumba Tandale au Mwananyamala, lakini si Marekani.


Nna nyumba South Africa kwa sababu nina familia South Africa kwa hiyo ni lazima ninunue nyumba south Africa, lakini sina sababu ya kusema
ninunue nyumba Marekani, ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani, kwanza sipapendi",
alisema Diamond.

Friday 8 April 2016

Meneja Wa Diamondi na TipTop Connection Ajibu Tuhuma zinazomkabili.

Meneja wa Diamond na Tip Top Connection.

Babu Tale amefunguka na kuzungumzia madai ya kuwa huwa anawabania baadhi ya wasanii wa nje ya management yake ili kuwapa nafasi wasanii wake.

Akizungumza katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Babu Tale amesema wale ambao wanasema kwamba wanabaniwa, wameshindwa kukiamini kile wanachokifanya ndio maana hawafanikiwi.

“Ukiwa na mentality kwamba Tale ndio anaendesha watu, mimi nilishawahi kukwambia piga ngoma hii,” Tale alimuuliza mtangazaji.

“Mimi sina radio wala TV. Unajua kila mtu ana mtanzamo wake, Ni kweli kuna watu wanasema mimi nimetawala muziki ni kweli, kwa sababu ngoma za wasanii wangu nilizotoa hivi karibuni ni kali, mimi kila siku nawaza media inataka kulipa kupiga ngoma, media haiwezi kulipa ngoma mbaya, kwa hiyo mimi nafikiria kesho,”

“Sijawahi kuwasimamia Weusi, lakini wanafanya vizuri kwenye muziki, mimi simsimamii Ommy Dimpoz na anafanya vizuri, ana jiamini na anafanya kazi yake katika ubora. Wapo pia ambao mimi nawasimamia na hawafanyi vizuri, kwa sababu hawajiamini na hawafanyi kazi nzuri.

Nipo kwenye team ambayo ina njaa na mimi mwenyewe nina njaa, sitaki kufanya kazi yangu tu ilimradi, wakati natoa nyimbo kama namtoa underground, hata kama natoa nyimbo ya Diamond naangaika kama namtoa ya underground,” aliongeza Tale.

Meneja Wa Mr Flevour apata mtoto miezi mnne tu tangu kuoa.

Mr Flavour
Meneja wa Msanii kutoka Nigeria Mr. Flavour bwana Benjamin Omesite na mkewe Ifeyinwa jana walibahatika kupata mtoto.Benjamin Omesite na mkewe Ifeyinwa walipata mtoto wa kike. Ikumbukwe wawili hawa walioana Mwezi Januari mwaka huu.


X-Girlfriend wa Wizkid ameshare picha za Arusi Yake.

Sophie Rammal

Sophie Rammal  Ameshare baadhi ya Picha za ndoa yake. 

Sophie Rammal ambae ni mpenzi wa zamani wa msanii Wizkid kutoka Nigeria amepost picha hizo akiwa katika mapozi tofauti na Mume wake anaejulikana kama Wale Alakija. Ndoa yao ilifungwa mwezi Januari Huko Lagos. 

Sophie Rammal Amekuwa akitrend sana kutokana na kushirikiana mambo mengi ikiwemo katika ”Holla at your Boy Music” Sophie na Wizkid waliDate kwa kipindi kifupi tu na kuachana. 

Tazama Picha Zaidi, 





Thursday 7 April 2016

Tanzia: Aliekuwa mbunge Viti maalumu Afariki Dunia


Dada ya Tundulisu na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita
katika hospitali ya Aga Khan Dar.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana.

Picha ya Diamond akiwa amevaa Hereni puani haimaanishi ametoboa pua.

Picha ya Diamond Platnumz ikimuanyesha akiwa na Hereni puani. (Picha na Mtandao)
Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua.

Ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo
Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki. "Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mklikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo


Maneno ya Meneja Sallam yanamaanisha kwamba sio kweli Diamond katoboa pua, ni mchezo tu na baada ya hiyo picha ya kutoboa pua Diamond aliweka picha nyingine inayoonekana hapa chini akiwa fresh kabisa.



Chanzo: Millard Ayo

Tommy Thomass: Mashabiki Mjiandae Mambo mazuri yanakuja



Msanii wa Hip Hop  kutokea mkoani Kilimanjaro Tommy Thomas amesema kitu kipya kitatoka Ndani ya mwezi huu.

Tommy Thomas akizungumza na BongoHomeTz amesema kwa sasa yupo katika hatua za mwisho ili aweze kuachia kibao hicho kipya.

"Kwa sasa nafanya makubaliano ya kibiashara na baadhi ya kampuni, ikiwemo Mkito na BongoHomeTz pia Cover na mambo mengine yanaelekea kukamilika. Hivyo Nadhani week ijayo nitatoa wimbo rasmi" Alisema Tommy Thomas.

Tommy Thomas aliitonya BongoHomeTz kuwa ngoma mpya inayokuja inaitwa "naongea" amemshirikisha becka title wa b.o b. Micharazo. studio ni Frezzo rec chin ya producer aidan machord

Kadhalika Aliongeza kuwa mara tu baada ya kutoa wimbo huo atakuwa na Media Tour katika media mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi.

Pamoja na hayo Thommy Thomas ametumia fursa hii kuwaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula. Kwa sasa Tommy Thomas Anatamba na Kibao alichomshirikisha Walter Chilambo kinachofahamika kama "Twende". Bofya hapa kudownload moja ya nyimbo kali za Tommy Thomas. (Tommy Thomas Ft Walter Chilambo-Twende MP3)

Sunday 3 April 2016

Mubba_C atua Singida kutambulisha nyimbo mpya.



Mkali wa Mistari kutoka Singida anaefanyia harakati zake Jijini Arusha Mubba_C amefanya ziara ndani ya Mkoa wa Singida kwa ajili ya kutambulisha kazi zake mpya.

Mubba_C ameiambia BongoHomeTz kuwa atatumia kituo cha redio cha Standard Redio kilichopo Mkoani Singida ili kufikisha kazi zake kwa maelfu ya mashabiki wake mkoani humo.

Wiki iliyopita Mubba_C alikuwa ndani ya jiji la Arusha akifanya utambulisho wa kazi zake mpya ambapo alihitimisha kwa kuzungumza Na mashabiki wake kupitia kipindi cha The Beat Show cha Arusha One FM radio.

Tayari ameshatambulisha nyimbo mpya ambazo zimepokelewa vizuri zikiwemo wimbo Nieleze, Hasoling Mapenzi kikohozi,Walisema na Wa Pekee

Hata Hivyo Mubba_C amewaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti kwa kuomba nyimbo zake kwenye vituo vya redio Na pia wahudhurie matamasha pale watakaposikia kuwa Mubba C anahusika.

NEW SONG| T.I.D ft Dully Sykes X Joh Makini - Confidence



                  DOWNLOAD HERE

New Song| Nikki Mbishi Ft Becka Title_Kwanini Mimi [Audio]



                         DOWNLOAD HERE

Monday 28 March 2016

Vanessa Mdee: Ninapovaa Nguo Fupi nina malengo haya


Muimbaji huyo ambaye ameachia video ya wimbo Niroge hivi karibuni, amekiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV kuwa, anapenda
kuvaa nguo fupi ili kutangaza brand yake, na hatimaye impe dili la matangazo kwa wabunifu wa mavazi.

Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past, wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao” alisema Vanessa

Aliongeza,”Mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili napigiwa simu na Balmain, na Louis Vuitton, nataka designers wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu kubwa na zinaendana, so nina malengo , na if I’m gonna offend anybody I’m sorry.”

Chanzo: Bongo5

Familia ya Rapper huyu yafikisha watoto Saba.


Rapper T.I. hataki mchezo.. Yeye na mke wake,Tiny wamepata mtoto wao wa saba.

Mtoto huyo wa kike alizaliwa wiki iliyopita. Taarifa hiyo ilitolewa na mtoto wa dada yake na T.I., Kamaya Harris.

My little cousin is here. Last night I went to go see my auntie and she had the baby today,” alisema kwenye Snapchat.

Watoto wengine wa familia ya Rapper huyo ni Messiah, Domani, Deyjah,King, Major na Zonnique.

Sunday 27 March 2016

Taarifa ya Chad kujiondoa #2017AFCON na Majibu wa mustakabali wa timu zilizosalia.


Taarifa za  timu ya Taifa ya Chad kujitoa kwenye mashindano ya AFCON zimekuja saa chache kabla ya kuvaana na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Mfano wa barua iliyobainisha Chad Kujitoa katika michuano ya #AFCON2017 (Picha na YerickoNyerere)


Baada ya kujitoa kwa timu hiyo sasa zitatumika kanuni za michuano hiyo zinazosimamiwa na CAF. Na huu ndio ufafanuzi wa hatma wa timu zilizopo kwenye kundi moja na Chad.

Kwa mujibu wa Kanuni sasa Matokeo yote ya Chad yamefutwa na hayatahusishwa na timu yoyote hata kama timu hiyo iliwahi kuifunga Chad na kujinyakulia pointi au kuwa katika nafasi iliyopo kutokana na magoli iliyoifunga Chad.

Kadhalika kundi litatoa mshindi mmoja ambae anashika nafasi ya juu zaidi kwenye kundi tofauti na makundi mengine yatatoa timu mbili za juu katika kundi.

Tweet kadhaa za CAF wakilitolea ufafanu sakata hilo la kujitoa kwa timu ya  Chad


Ikumbukwe Chad ilikuwa katika kundi G na Nigeria, Misri (Egypt) na Tanzania, Taifa Stars.

Siri ya maisha ya wasanii waliopo kwenye Lebo ya WCB. Harmonise Amefunguka.



Msanii kutoka lebo ya WCB Harmonize, ametoa siri ya maisha ya wasanii ambao wako chini ya lebo hiyo, ambayo inawafanya kuepuka mambo mengi ikiwemo skendo chafu, huku akidai kuwa wanafuata nyayo za bosi wao Diamond Platnums.

Harmonize ameongea hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kuwa wao kama WCB hawana kawaida ya kwenda club kutokana na kubanwa na majukumu, na pia hata bosi wao ambao ni mfano mzuri kwao, hana kawaida ya kwenda sehemu kama hizo.

“Labda nizungumze kitu kimoja, WCB sio mimi tu hata wasanii wengine ambao watatoka WCB kuna life style ambayo watafuata, lakini mimi kama mimi sipajui club kabisa, sijawahi kwenda club sitokagi, kwa sababu pale ofisini kuna studio studio mle mle ndani, kuna vyumba ambavyo ukirekodi ukichoka unakaa unarefresh mind, kuna game station mnakaa mnacheza game, alafu pia kuna vyumba vya kuishi mule mule, muda wenyewe wa kutoka unakosa, alafu pia ukizingatia CEO mwenyewe wa WCB hana hizo mambo za kwenda club, so sisi tunajifunza kupitia yeye”, alisema Harmonize.

Pia Harmonize amekiri kuwa umaarufu alionao sasa ndio unamfanya ashindwe kwenda sehemu mbali mbali pamoja na kujichanganya na wasanii wengine, kutokana na kutozoea mazingira hayo, huku akitamani maisha aliyokuwa nayo kabla, lakini pia kuna muepusha na skendo mbaya.

Juzi kulikuwa na mwaliko Mh Rais alialika wasanii Ikulu, mi sikuenda kwa sababu sijazoea hayo mazingira, kwa hiyo inakuwa ngumu kuhusishwa na skendo huyo mwanamke nakutana nae wapi, sababu muda wa kutoka nakuwa sina, mi sikutanagi na wasanii wenzangu yani, muda naukosa kabisa, na ndo kati ya vitu ambavyo navimisi kabisa”, alisema Harmonize.


Chanzo: UdakuSpecially

Saturday 26 March 2016