Monday 29 February 2016

Mbowe akosoa operesheni tumbua majipu

Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai Mh. (mb) Freeman Mbowe (picha na Maktaba)

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amekemea kile alichokiita “fukuza fukuza” ya watumishi wa umma bila kufuata taratibu.

Kauli ya Mbowe imekuja wakati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, ikiwa katika kampeni ya kufukuza na kusimamisha watumishi wa umma wanaotuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu, wizi, uzembe na njama za kuhujumu mapato.

Operesheni hiyo inafanyika kwa kuwasimamisha kazi watumishi hao huku uchunguzi ukiagizwa kufanywa wakati tuhuma zao zikiwa zimeshatajwa hadharani.

Tayari watumishi zaidi ya 160 wameshasimamishwa au kufukuzwa kazi tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani. Kati yao, tayari wachache wamefikishwa mahakamani.

Mbowe alisema ufukuzaji watumishi wa umma bila ya kufuata taratibu hautakiwi na kuwataka viongozi wa dini kukemea mwenendo huo.

Alitoa kauli hiyo mbele ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo katika ibada maalumu iliyofanyika kwenye usharika wa Nshara wilayani Hai.

Ibada hiyo, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali, ilikuwa ni kwa ajili ya uzinduzi wa ukarabati na upanuzi wa jengo la Kanisa la Bethel lililopo katika Usharika wa Nshara.

Mbowe alisema hadi sasa, zaidi ya watumishi 160 wa Serikali wamefukuzwa au kusimamishwa kazi bila Serikali kuweka wazi makosa yao, huku familia za baadhi yao zikiendelea kutaabika.

Mbali na suala hilo, aliwataka viongozi wa dini kuingilia kati mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ambako alisema dhana ya demokrasia haifuatwi kama viongozi wa Serikali wanavyodai.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Shoo hakujikita kuzungumzia suala hilo, badala yake alijielekeza zaidi kwenye uharibifu wa mazingira.

Askofu Shoo alisema licha ya Tanzania kuwa na Sheria nzuri za kudhibiti mazingira, hazifuatwi hali inayosababisha asilimia 60 ya eneo la nchi kuwa jangwa.

Askofu alisema kutofuatwa kwa sheria hizo kumesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kusababisha majanga kwa baadhi ya maeneo yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Dk Shoo alisema kumekuwapo na mafuriko ya mara kwa mara, kutokana na wananchi kutozingatia kilimo bora hali inayosababisha mmomonyoko wa ardhi, ikiwa ni pamoja na ardhi kupoteza rutuba.

“Wananchi wamekuwa wakitumia sumu katika vyanzo vya maji hali inayosababisha vyanzo vingi kukauka na Kilimanjaro ni miongoni ya maeneo ambayo yanatajwa kuwa jangwa,” alisema Askofu Shoo.

Askofu Shoo alisema tafiti mbalimbali na zinaonyesha ukataji wa misitu umesababisha uharibifu mkubwa hivyo ni vyema Serikali ikachukua hatua za haraka ili kuokoa kizazi kijacho.

Aliwataka wananchi kuchukua hatua za haraka kutunza mazingira hususan miti ya asili ambayo inaweza kusaidia kurudisha uoto wa asili ambao tayari umeharibiwa baadhi ya maeneo.

Katibu wa kamati ya ukarabati na upanuzi wa kanisa hilo, Endrey Uronu, alisema zaidi ya Sh1.5 bilioni zinahitajika katika ujenzi huo huku katika harambee iliyofanyika jana, Sh279 milioni zilipatikana.

Cheka: Nimeshinda ila kwa mbinde sana.

Ajetovic mwenye asili ya Serbia akipokea pande la ngumi kutoka kwa Bondia Fransis Cheka

Pamoja na kutwaa taji la mabara la WBF, Francis Cheka amekiri ushindi wake ameupata kwa mbinde kutokana na ubora wa mpinzani wake Geard Ajetovic katika pambano lao lililofanyika usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi, Cheka alisema mpinzani wake alimsumbua sana.

“Nimeshinda, lakini nakiri ni kwa mbinde mpinzani wangu alikuwa mbishi, amenipa wakati mgumu kwa kweli. Sikutarajia upinzani huu. Lakini nashukuru nimeshinda,” alisema Cheka.

Katika pambano hilo la raundi 12 lililosimamiwa na Rais wa WBF, Goldberg Haward, bondia Geard Ajetovic alicheza kwa kudhamiria kutwaa taji hilo hakumpa mwanya Cheka katika raundi ya tano hadi ya nane, hivyo kuwalazimu mashabiki wa Cheka kukaa kimya kwa dakika sita za raundi hiyo na wakuwapa nafasi mashabiki wachache wa Ajetovic.

Cheka alibadili raundi ya tisa na kumi huku raundi ya 11 na 12 mabondia hao wakicheza kwa kuviziana kabla ya Cheka kutangazwa bingwa kwa majaji 3-0. Jaji namba moja, Sakwe Mtulya alimpa Cheka pointi 115-112 wakati Anthony Rutha akitoa pointi 116-111 kwa Cheka na jaji namba tatu akitoa pointi 115-112 kwa Cheka kabla ya refarii kutoka Afrika Kusini, Eddie Marshall kumtangaza Cheka kuwa bingwa wa taji hilo katika uzito wa super middle.

Cheka ambaye yuko chini ya Kampuni ya Advanced Security Company Limited chini ya Mkurugenzi wake Juma Ndambile ambaye ni meneja wake, angeweza kupigwa kwa TKO kama si uvumilivu wa kucheza na kumaliza raundi zote 12 licha ya kupasuliwa na Ajetovic raundi ya nane na Ajetovic.

Akizungumzia ushindi wa Cheka, Ajetovic mwenye asili ya Serbia alisema mpinzani wake alipendelewa na kusisitiza yeye ndiye alistahili kushinda lakini uenyeji umembeba
Cheka.

“Nilistahili kushinda, lakini siwezi kupingana na uamuzi wa majaji, bado sijaamini kama nimepigwa na Cheka, Niko tayari kurudiana naye,” alisema bondia huyo aliyeambatana na kocha wake, Aksu Ahhysaidar

List ya washindi wa tuzo za Oscar 2016

Tuzo za Oscar 2016 zimefanyika nchini Marekani. Bongo Home Tz wameona ni vyema ukipata list nzima ya washindi.

Baadhi ya washindi wakipongezana mara baada ya kutangazwa washindi wa tuzo za Oscar

Best original screenplay – SPOTLIGHT

Best adapted screenplay – THE BIG SHORT

Best supporting actress – Alicia Vikander, The Danish Girl

Best costume design – MAD MAX: FURY ROAD

Best production design – MAD MAX: FURY ROAD

Best make-up and hair – MAD MAX: FURY ROAD

Best cinematography – THE REVENANT

Best editing – MAD MAX: FURY ROAD

Best sound editing – MAD MAX: FURY ROAD

Best sound mixing – MAD MAX: FURY ROAD

Best visual effects – EX MACHINA

Best animated short – BEAR STORY

Best animated film – INSIDE OUT

Best supporting actor – MARK RYLANCE, BRIDGE OF SPIES

Best short documentary – A GIRL IN THE RIVER: THE PRICE OF FORGIVENESS

Best documentary – AMY

Best short film – STUTTERER

Best foreign language film – SON OF SAUL

Best original score – ENNIO MORRICONE, THE HATEFUL EIGHT

Best original song – WRITING’S ON THE WALL, SPECTRE

Best director – ALEJANDO GONZALEZ INARRITU, THE REVENANT

Best actress – BRIE LARSON, ROOM

Best actor – LEONARDO DICAPRIO, THE REVENANT

Best picture – SPOTLIGHT

Chanzo: Dewjiblog

Sunday 28 February 2016

Makonda: Walimu bure kusafiri Dar

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala (DARCOBOA), Sabri Mabrouk na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Daladala (Uwadar), William Masanja, kulia. 



Pengine hii yaweza kuwa ni historia; kuanzia Machi 7 walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaofundisha shule za Serikali za msingi na sekondari, hawatalipa nauli kwenye kwenye daladala wakati wakienda na kutoka kazini.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alitangaza hayo jana mbele ya viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria na madereva Mkoa wa Dar es Salaam.

Makonda alisema wazo lake la kutaka walimu wasafiri bure limeungwa mkono na viongozi wa vyama vya wasafirishaji abiria na wamiliki wa daladala na kwamba kilichobaki ni kuanza kutoa huduma hiyo.

“Awali, wazo langu ilikuwa walimu wa Wilaya ya Kinondoni ninayoiongoza, ndiyo wafanyiwe utaratibu wa kusafiri bure lakini wadau wa usafirishaji wakashauri iwe kwa mkoa mzima. Nikamweleza mkuu wa mkoa na akaniruhusu tufanye hivyo mkoa mzima,” alisema Makonda ambaye mpango wake wa kuchangia ujenzi wa shule umemhakikishia cheo baada ya Rais John Magufuli kuguswa.

Makonda alisema kuanzia leo, wakuu wa shule za msingi watakakiwa kuwatengenezea walimu wao vitambulisho kwa ajili ya usafiri.

Alisema vitambulisho hivyo ambavyo vitavaliwa wakati wa kupanda daladala, vitatakiwa kuwa na picha ya mwalimu, jina lake kamili na jina la shule anayofundisha.

Mkuu wa wilaya hiyo alisema vitu vingine vinavyotakiwa kuwa kwenye vitambulisho hivyo ni saini ya Makonda ili kuepuka udanganyifu na namba ya simu ya mkuu wa shule husika.

Alisema baada ya vitambulisho kukamilika, walimu watapanda bure katika daladala lolote wakati wa kwenda kazini kuanzia saa 11.30 hadi saa 2.00 asubuhi na kwamba wakati wanarejea nyumbani huduma hiyo itaanza saa 9.00 alasiri hadi saa 11.00 jioni.

Makonda alisema huduma hiyo ya usafiri bure kwa walimu itatolewa siku tano kwa wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na kwamba siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu watatakiwa kulipia.

“Huo ni muda ambao wamiliki wamekubali kusafirisha walimu bure kwenda kazini na kurudi nyumbani. Nje ya muda huo walimu watatakiwa kulipa nauli kama kawaida,” alisema.

Makonda alisema baada ya Rais Magufuli kutangaza elimu bure, aliona amuunge mkono kwa kuweka mazingira yatakayorahisisha utendaji kazi wa walimu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala cha Dar es Salaam (Darcoba), Sabri Mabruki alisema wamekubali kutoa usafiri bure kwa walimu ili kumuunga mkono Magufuli katika juhudi zake za kuboresha elimu. “Tumeletewa ombi na mkuu wa wilaya akitueleza kuhusu wazo la kutaka kusafirisha walimu bure. Kwa namna Makonda na Rais wanavyofanya kazi, hatukuwa na kinyongo zaidi ya kukubali ombi hilo,” alisema.

Akiunga mkono huduma hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria (Uwadar), William Masanja alisema elimu bure haiwezi kufanikiwa kama mazingira ya kazi ya walimu yatakuwa magumu.

“Ndiyo maana tulivyoambiwa na mkuu wetu wa wilaya, hatukuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kukubali ombi lake. Tumejipanga kuwasafirisha walimu ili waweze kufundisha watoto wetu,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama Wafanyakazi Madereva Tanzania (Tadwu), Shaaban Mdemu aliwataka walimu kuzingatia muda uliopangwa kusafiri bure ili kuondoa usumbufu.

Aliwataka wamiliki wa daladala kuwa wasikivu iwapo wataambiwa na madereva wao kuwa mapato ya siku yamepungua kutokana na kuwepo kwa huduma hiyo.

Akizungumzia uamuzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch alisema jambo hilo likitekelezeka, Makonda atakuwa kiongozi wa mfano hapa nchini kuthamini kazi za walimu.

“Mpango huu unatakiwa kupongezwa, kuungwa mkono na wadau wa elimu. Tunahitaji kuwapa moyo viongozi wabunifu kama hawa,” alisema.

Alisema walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatumia wastani wa Sh3,000 kwa siku kwa ajili ya usafiri wa daladala.

“Sehemu kubwa ya mishahara ya walimu inatumiwa kwa ajili ya usafiri, mpango huu utakuwa mkombozi kwao,” alisema.

Alisema kama mpango huo utafanikiwa mkoani Dar es Salaam, unatakiwa kuanzishwa kote nchini.

Hata hivyo, Oluoch alipendekeza mpango huo utungiwe kanuni ili makubaliano hayo yaendelee kudumu hata kama viongozi hao hawatakuwepo Dar

Masaju: Muswada wa sheria ya kuanzishwa mahakama ya mafisadi umekamilika

George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema Miswada ya marekebisho ya Sheria ipo jikoni ambapo mabadiliko hayo yataisaidia serikali kutimiza ahadi  zake.

Kadhalika Masaju amesema mswada wa sheria ya kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi uko tayari na utawasilishwa Aprili mwaka huu bungeni, kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria, kutoa nafasi kwa mahakama hiyo kuanza kazi.

Ikumbukwe kuwapo kwa mahakama ya mafisadi ni ahadi ya mh. Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa alipokuwa akijinadi katika kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Mwaka jana Oct 25.

Chanzo: EATV

Shomari Kapombe mchezaji bora ligi kuu Vodacom mwezi Januari



Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016.

Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016.

Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, na mara nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake.

Washindani wa Kapombe kwenye kinyang'anyiro hicho katika mwezi huo walikuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam.

Kwa kutwaa tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Limited.


Chanzo: TFF

Mh. Raisi Magufuli Tayari yupo Jijini Arusha

Mh Rais John Pombe Magufuli Akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari.
Tayari Mh. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amekwishafika Jijini Arusha Kuongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini hapa.

Mh. Raisi aliwasili Katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (K.I.A) majira ya asubuhi ya leo tar 28 Feb 2016.

Kadhalika Mbunge wa Arumeru Mashariki mh. (mb) Joshua Samwel Nassari ni miongoni mwa viongozi na wananchi waliojitokeza kumlaki mh. Rais.

Diamond kuachia wimbo mpya soon uitwao Simba




Staa wa muziki Diamond Platnumz amejipanga kuachia wimbo mpya wa kurap uitwao Simba.

Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Meneja wa msanii huyo, Babu Tale alisema wimbo huo utakuwa sio wa biashara bali ni zawadi kwa mashabiki.

“Kama Hip Hop ni biashara Diamond amefanya wimbo wa kurap lakini hatujauchulia kama ile ni biashara, wimbo umeshaisha na unaitwa Simba,” alisema Babu Tale.

Diamond kwa sasa anafanya poa na video ya wimbo ‘Make Me Sing’ akiwa na AKA wa Afrika Kusini.

Saturday 27 February 2016

New Video: Nay Wamitego-Shika adabu yako


New Video: Nay Wamitego- Shika Adabu Yako

     DOWNLOAD HERE

Download New song kutoka kwa MO Town Star- Nikuache Uende


Huu hapa wimbo wa msanii anaechipukia kwa kasi sana kutokea Kilimanjaro Mo Town Star- Nikuache Uende ndio wimbo anaotamba nao kwa sasa.

    DOWNLOAD HERE

Tuesday 23 February 2016

Penzi la Wema kwa Idrisa mashakani. Wema amechukua Uhamuzi huu

Penzi donda ndugu, ndio msemo pekee unaoweza kuupachika katika kipindi kama hiki cha migogoro ya mahusiano.
Japo hatujafahamu hasa chanzo ni nini, na nini hasa kimetokea lakini dalili za awali tu zinaonesha penzi kati ya muigizaji Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother Idriss Sultan limefika kikomo.
Vita ya maneno kati ya wawili hawa, iliibukia mitandaoni huku kila mmoja akirusha vijembe kwa mwenzake.
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mastaa hawa wamelivunja penzi lao mapema mno, huku mwanadada Wema Sepetu akionekana muhanga zaidi kwani amefuta picha zote za Idriss alizowahi kupost mtandaoni Instagram.
Matatizo kati yao yameanza kuibuka tangu siku ilipowekwa wazi kuwa, Ujauzito wa Wema umeharibika.

Mo Music afutiwa kesi ya utapeli,alimtapeli nani,ilikuaje?


Mo-music
Mahakama ya mjini Dodoma imefuta kesi ya utapeli iliyokuwa ikimkabili Msanii wa bongo Fleva,Mo music ambapo msanii huyo alikuwa akituhumiwa kama mtuhumiwa wa pili.
Kesi hiyo iliibuka baada ya mpenzi wa zamani wa Mo Music kumtapeli mwanaume mmoja anayesadikiwa kuwa ni mpenzi wake mpya pesa zaidi ya shilingi milioni 30 mwishoni mwa mwaka jana huko dodoma na kuaminika kuwa alimpelekea msanii huyo pesa hizo.
Mo Music amekana na kusema si kweli kwamba alicheza mchezo huo na mpenzi wake wa zamani na kuongeza kuwa mwanamke huyo amekuwa akimletea kadhia mara kwa mara hasa pale anapotaka kutoa wimbo hata kufikia hatua ya kuzusha kuwa ana ujauzito wa msanii huyo.
Chanzo:Ayo Tv

Dogo Janja kutoa wimbo mpya?hiki ndicho kinacho trend kuhusu yeye..




Baada ya siku chache Madee kuthibisha kuwa kulingana na kalenda ya Tip Top mwezi wa pili ni wa Dogo Janja kutoa wimbo,mambo yameshaanza kunukia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Janja amepost picha yake iliyoandikwa “Mtazidi Kupenga Kisa Stress Mpaka totorojanja
Picha hiyo imekuwa ikipostiwa na mastaa mbali mbali kuonesha kwamba kuna kitu kinakuja,kama ilivyo desturi ya wasanii wanapotakana kutoa wimbo. janja3


janja2

Simu yamfanya bodaoda kulivaa Lori, Inasikitisha sana hii imetokea Moshi


Tabia ya kudharau sheria za usalama barabarani imegharimu maisha ya mwendesha bodaboda, baada ya kulivaa kwa mbele lori aina ya Scania, alipokuwa akiongea kwenye simu huku akiendesha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhani Mungi alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 jioni, katika barabara ya Arusha- Moshi.
Kamanda Mungi alimtaja marehemu ni Joseph Asenga(30) mkazi wa Bonite na alisema mtu huyo aliyekuwa akiendesha pikipiki alikuwa akitokea Bonite alilivaa lori, wakati akijaribu kuhama upande wake huku dereva wa lori naye akijaribu kuhama upande wake ndipo walipogongana.
“Katika tukio hilo inaonekana kuwa dereva wa pikipiki na dereva wa lori wote waliokuwa wanakwepa, yaani kutaka kuyapita magari yaliyokuwa mbele yao ndipo walipokutana uso kwa uso hivyo kupeleka huyu dereva wa pikipiki kuingia chini ya lori na kugongwa,” alisema Mungi.
Alisema kuwa baada ya ajali hiyo dereva wa pikipiki alifariki dunia muda mchache, kabla ya kupewa matibabu katika hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.
Mashuhuda wa ajali hiyo Hamisi Mussa na Vicky Kimario, walisema kuwa dereva wa bodaboda alikuwa akizungumza na simu yake ya mkononi bila kutarajia kitakachotokea. “Hawa bodaboda ni wazembe sana, huyu kaka alikua anachati tangu nilipomuona mbele yangu, hakuwa na akili ya kuwaza kilichopo mbele yake akaingia chini ya lile lori na kupoteza maisha hapo hapo,” alisema Hamisi Mussa.
Vicky Kimario mkazi wa Moshi alisema wakati akivuka barabara alishuhudia bodaboda ikiingia chini ya lori na hatimaye aliyekuwa akiendesha hakutoka alikuwa ameshafariki dunia. “Simu ilimponza yule jamaa, alishindwa kujisaidia wakati wa tukio kwakuwa alinogewa na maongezi ya simu aliyokuwa akiwasiliana nayo, bila kujua wakati navuka barabara nilistaajabu kuona ameshakuwa maiti,” alisema Kimario.

Kama bado hujapata ratiba ya fainali za Copa America Nimekuwekea hapa.





16_CAC_GEN_GGL

Michuano hii itachezwa katika viwanja 10 tofauti vyenye tofauti vyenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 50,000/= kila mmoja.

Kadhalika Fainali itachezwa juni 26 katika kiwanja MetFire stadium.

14561071679577

Nimekuwekea Maneno ya Roma Mkatolki kuhusu uhandaji wake wa video.


roma
Msanii wa Hip Hop nchini Roma amefunga na kusema kuwa kwa sasa hafikirii kwenda kufanya video nje ya nchi kama wasanii wengi wanavyodhani kwani anaamini kuwa soko lake liko ndani zaidi hivyo kufanya hivyo kunaweza kumpa hasara tu.
Roma amesema kwa sasa anajenga misuli ili wakati ukifika wa kufanya muziki wake kimataifa umpatie faida zaidi kwa kuwa atakuwa amefanya kazi kulenga soko fulani na atafanya kulingana mahitaji ya soko hilo.
Mimi naangalia soko langu lilipo..me naangalia sana swala la mkwanja hiyo inanipa hofu.huwezi ukaenda ku shut nje halafu unataka soko lako liwe Dar Live.Unashangaa msanii anafanya hivyo lakini sijawahi kumsikia akifanya show Nigeria au south Afrika” amefunguka Roma na kusema kuwa target ya kwa sasa ni Tanzania

.

Banana Zoro Leo amefunguka siri kati yake na Msanii Maua Sama.Soma hapa full story


banana-zorro
Msanii mkongwe Tanzania Banana Zoro amefunguka na kusema kuwa anatamani sana kufanya kazi na mwanadada anayetamba na kibao chake cha Mahaba Niue,Maua Sama.
Banana amesema kuwa Maua ni msanii ambaye hatabiriki na anaweza kuimba aina tofauti tofauti za muziki na kukiri kuwa hajawai kumwambia mwenyewe sifa hizo kwa kuwa hajapata nafasi bado ya kukaa naye chini.
Maua ana fusion.Anaweza akaimba zouk vizuri,R&B,Sweet raggae,anabadilika badilika huwezi kumtabiri kwenye staili moja” alifunguka Mkongwe huyo na kusema yuko mbioni kufanya kazi na wasanii wa kimataifa japo hakutaka kuwataja.
Source: Radio 5

Monday 22 February 2016

Kikosi cha polisi cha wanamaji Tanzania kimekamata Jahazi likiwa limesheheni bidhaa tofauti na zinazoonyeshwa na kibali.




Kikosi cha Polisi cha wanamaji kimekamata jahazi likiwa linatokea bandari ya Zanzibar kwenda bandari ya Dar es Salaam likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo spika za redio na friji wakati jahazi hilo liliondoka bandari ya Zazibar kibali chake kikionyesha kuwa limebeba mafuta ya marashi.
 
ITV ilifika makao makuu ya kikosi hicho na kukuta jahazi hilo linaloitwa Najat likiwa limejaa vifaa hivyo huku polisi na wafanyakazi wa jahazi hilo wakisaidia kushushwa kwa vifaa hivyo ambapo kamanda wa kikosi hicho Semboje Kanga amesema nyaraka za mzigo haziendani na kilichobebwa.
 
Katika hatua nyingine wenye mzigo huo wamejitokeza na kusema kuwa wananyaraka zote muhimu na wanashindwa kuelewa kwa nini polisi wanasema shehena hiyo wanamashaka nayo.
 
Naye mliki wa chombo hicho kilichokamatwa Bw Iddy Hadibu amesema kilichotokea ni kwamba wakati wanakuja bandari ya Dar es Salaam baharini wakakuta chombo kingine kimelemewa na mzigo na ndio wakawasaidia ili wasipate shida na hapo ndipo walipojikuta wanaingia katika dhahama hiyo.


Chanzo: ITV Tanzania

Hili ni wazo la Ray Kigosi baada ya kuona ishu ya maji imekuwa gumzo kila kona.

Ray_-_bongomovies
Baada ya kauli ya msanii wa bongo muvi Ray kigosi kuwa gumzo kila kona msanii huyo amesema amepata wazo la kufanya biasahra kupitia kiki hiyo.
Ray amesema amepata mawazo kutoka kwa watu wengi na yeye yuko kwenye mpango wa kuzungumza na makampuni yanayouza maji ili aweze kuyatangaza au anaweza kutengeneza documentary inayoelezea umuhimu wa kunywa maji na kuomba air time kwenye vituo vya televisheni
Nimepata mawazo kutoka kwa watu wengi,ulaya ingekuwa ni kitu kikubwa lazima makampuni yangenifuata niwafanyie matangazo lakini kwetu Afrika bado..naweza kwenda kampuni yoyote kuomba sponsorship nikapata au kutengeneza documentary ya umuhimu wa maji nikapeleka kwenye TV nikapata pesa” alifunguka Ray ambapo wiki iliyopita alisema anakunywa sana maji ndio mana anakuwa mweupe kufanya kauli hiyo kuwa gumzo kwenye mitandao.

Baada ya kusikia video ya Zigo Rimix Imefungiwa kchezwa katika televisheni hii hapa kauli ya AY kwa TCRA

Ay diamond
Baada ya kuwepo taarifa kuwa video ya A.Y,Zigo aliyomshirikisha Diamond imefungiwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kutokana na kutokuwa na maadili,msanii huyo amekiri kupokea barua kutoka kwa mamlaka hiyo.
Hata hivyo AY ameshangaa hatua hiyo na kuhoji ni maadili yapi ambayo hayajazingatiwa kwenye video hiyo,na pia mbona hawafungii video za nje ambazo zinakiuka maadili zaidi.
Unajua unavyo shoot una shoot kama maudhui ilivyo,huwezi ukavaa suti jangwani au ukavaa overall kwenye swimming pool..na mavazi ya swimming pool yako kila sehemu hata katika taarifa ya habari tunayoona kwenye vipindi vya michezo kama wao pia wanakiuka habari nitakubaliana nao..kama wanafungia wimbo wa zigo na kuacha za kina nick minaj ni sawa kama wanaona maadili ya kina Nick Minaj yako sawa na kina Ay ndo mabaya,inabidi kukubaliana nao” alifunguka AY
Hata hivyo Innocent Mungi kutoka TCRA hakutaja moja kwa moja kuwa video hio umefungiwa bali wametoa barua kwenda kwa vituo vinavyorusha matangazo ya Tv kuwa wasimamie kanuni za maudhui ya utangazaji kusitisha kurusha nyimbo zote zinazokiuka kanuni hizo.
Source: Clouds

Mabibi na mabwana hapa nimewawekea taarifa kamili kuhusu Waziri Kairuki kutumbua majipu


Mawaziri wa Magufuli wameendelea kumiliki vichwa vya habari  kutawala katika Wizara mbalimbali Tanzania ambapo leo imegusa katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ambapo Waziri wake Angellah Kairuki ametangaza kuwaondoa kazini watumishi watatu kwa ubadhirifu wa mali za Umma.
Amesema ‘namsimamisha kazi Said Nassoro aliyekua mkuu wa chuo cha utumishi wa Umma kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake na kushindwa huko kusimamia kikamilifu, kumepelekea shughuli za matawi ya chuo hiki mikoani kuathirika na kutoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhirifu wa mali za umma’
‘Kuanzia mwaka 2011 mpaka 2013 mkuu wa chuo tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la gorofa mbili katika tawi letu la chuo huko Mtwara, CAG na TAKUKURU walithibitisha ubadhirifu huu lakini mkuu huyu wa chuo niliyemsimamisha hakuchukua hatua na badala yake alimuhamishia Ngata Tabora na kuendelea na wadhifa wake’
Waziri Kairuki ameeleza pia ‘Ngata naye anasimamishwa kazi, na wa tatu ni Mbwilo Joseph ambaye mwaka 2013 alitumia vibaya pesa za malipo ya ada Bilioni moja zilizolipwa na Wanafunzi ambapo pamoja na ubadhirifu huo kugundulika bado mkuu wa chuo Nassoro alimteua kuwa kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa utawala na fedha, naye kuanzia leo anasimamishwa’

Rooney kweli kiboko, Soma uhamuzi yake kuhusu kuhama Man U au kusalia.



Rooney24

Klabu ya Shanghai Shenhua ilianza kuiomba Man United kumsajili Wayne Rooney kwa dau la pound milioni 27 mwishoni mwa mwaka 2015, kwa sasa inamuhitaji na ilikuwa inataka kumlipa mshahara wa pound 500,000 kwa wiki, kwa mkataba wa miaka mitatu, huu unakuwa ni mshahara ambao ni mara mbili ya anaopokea Man United ambapo angekuwa Wayne Rooney anavuna zaidi ya Tsh bilioni 220 kwa kipindi cha miaka mitatu nje ya posho na bonansi za mechi.
Sunday Times iliripoti February 20 kuwa Wayne Rooney alikataa mpango huo wa kujiunga na klabu hiyo ya China. klabu ya Shanghai Shenhua iliwahi kuwasajili wachezaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na Nicolas Anelka, Hivyo Rooney kukataa dili hilo la kujiunga na klabu hiyo unafananishwa sawa na Rooney kukataa zaidi ya Tsh bilioni 220

Tamisemi yawataka watendaji mkoani Arusha kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Soma zaidi








Naibu waziri wa Tamisemi Bw.Suleimani Jaffo amemtaka katibu  tawala wa mkoa wa Arusha kumpatia orodha ya watendaji   wanaoendelea  kufanya  kazi  kwa  mazoea na kusababisha wananchi   kuteseka  bila  sababu  za  msingi  ili  hatua  zikiwemo za kuwafukuza  kazi zichukuliwe  haraka  kwani  wakati wa kubembelezana umekwisha.

Mh.Jaffo  ameyasema hayo baada ya kupewa taarifa inayopingana na  hali halisi ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali likiwemo la  kushughulikia  maafa yanayowapata wananchi iliyosababisha baadhi ya  watendaji kushindwa  kujieleza na wengine kutupiana lawama na  kuikana  maelezo yao wenyewe.
 
Mkanganyiko  wa watendaji hao ulikuja baada ya naibu waziri Mh.Jaffo  kutaka kupata maelezo ya  watendaji  hao wanavyoshughulikia  majanga   mbalimbali yanayowapata wananchi likiwemo la kuezuliwa kwa shule  ya msingi isimani lililotokea Desemba mwaka jana ambalo hadi sasa  hatua hazijachukuliwa licha ya kuwa ndani ya uwezo.
 
Katika sakata hilo kadiri viongozi na watendaji hao walivyojaribu kutoa maelezo yaliendelea  kutofautiana jambo ambalo Mh.Waziri.Jaffo  amesema linalodhihirisha wazi kuwa lipo tatizo ambalo serikali   haiwezi kuendelea kulifumbiwa  macho.
 
Mh.Naibu waziri Suleiman Jaffo alifanya ziara ya kushtukiza  mkoani  Arusha ambayo inadaiwa kuwa ni matokeo ya malalamiko ya wannachi  wakiwemo wanaopatwa na maafa ama majanga mbali mbali ya  kuchelewa kupata  msaada wa serikali licha ya kupewa ahadi kila janga  linapotokea.

Napenda ufahamu kuwa Ney Wamitego anatarajia kutoa video ya Shika adabu yako..Bofya Link kupata habari kwa undani

Licha ya audio wa wimbo wake wa shika adabu yako kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) rapper Nay Wa Mitego ameweka wazi kuwa ataachia video ya wimbo huo ijumaa ijayo ya tarehe 26 februari.

Kupitia akaunti yake ya Instagram rapper huyo ambaye kwenye wimbo huo amewashambulia kwa maneno watu mbalimbali maarufu ameweka picha na kuandika “#ShikaAdabuYako 26Feb video inatoka.! Ijumaa hii.! #ShikaAdabuYako” kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

nayy wa mitego

Sunday 21 February 2016

Baada ya matokeo ya uchaguzi nchi Uganda kutangazwa hiki ndicho kilichomkuta Dkt. Kizza Besigye Leo




Dkt. Kizza Besigye, amekamatwa na polisi asubuhi hii nyumbani kwake Kasangati, hii imetokea baada ya Polisi wa kutosha kuizingira nyumba yake kufuatia taarifa za kuwepo maandamano kwenda Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi (EC) kuwasilisha fomu za matokeo ya uchaguzi amabazo matokeo yake yanatofautiana na matokeo yaliyotangazwa na Tume hiyo.

NBS Television. Kupitia ukurasa wao wa facebook wameweka hujumbe huu hapa.


Ne-Yo Anatarajia kupata mtoto wa kwanza pia kuna story nyingine kuhusu ujio wake hapa Tz

Muimbaji wa R&B, Ne-Yo amefunga ndoa na mchumba wake Crystal Renay.
ne-yo-1024
Harusi yao ilifungwa Jumamosi mbele ya wana familia na marafiki huko Rancho Palos Verdes, Los Angeles, Marekani.
“Tuna hamu ya kuanza maisha pamoja,” Ne-Yo aliliambia jarida la People. “Tunatarajia kuwa marafiki wa dhati.”
Wamefunga ndoa wakati ambapo wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.
Ne-Yo tayari ana watoto wawili, wa kike Madilyn Grace, 5, na wa kiume Mason Evan, 4 kutoka kwenye uhusiano wa zamani.
Muimbaji huyo anatarajiwa kutumbuiza jijini Mwanza, May 21

Jecha amkana Maalim Seif na washirika wake.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akizungumza. Picha na Maktaba 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, ameibuka tena na kutangaza kukamilika kwa matayarisho ya uchaguzi wa marejeo Machi 20, mwaka huu huku akikataa kutoa majina ya wagombea.
Jecha ambaye tangu afute uchaguzi alionekana hadharani Januari 12, 2016 wakati wa sherehe za Mapinduzi na baadaye kwenye televisheni akitangaza tarehe ya uchaguzi huo wa marudio, alisema wagombea wote ‘waliojitoa’ watapewa haki zote wanazostahiki kupewa kama wagombea kwa kuwa hawakufuata taratibu za kisheria za tume hiyo akimaanisha kuwa hakuna mgombea aliyejitoa kauli ambayo inapingana na msimamo wa CUF ambayo imetangaza kuwa mgombea wake wa urais Maalim Seif Sharif Hamad hatagombea.
Kama alivyofanya wakati anatangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio, jana alizungumza kupitia mwandishi wa Televisheni ya Taifa (TBC), akiwaacha waandishi waliokuwa wameitwa kwa ajili ya mkutano wake nje ya ofisi hiyo.
Jecha ambaye amekuwa haonekani hadharani isipokuwa katika matukio machache, alisema tume yake inawahesabu waliokuwa wagombea katika uchaguzi uliofutwa kuwa ni halali, licha ya kuandika barua za kujitoa katika tume hiyo. “Pamoja na kuwa wagombea wengi, hasa wa CUF, kuandika barua za kujitoa katika ofisi za ZEC wilaya na makao makuu, hakuna barua hata moja ambayo imefuata utaratibu wa kisheria na kwa mantiki hiyo, bado tunahesabu wagombea hao ni halali katika uchaguzi mkuu wa marejeo,” alisema Jecha. Katika taarifa hiyo, Jecha alisema vyama vinane vimeshathibitisha ushiriki wake katika uchaguzi huo vikiwamo Tadea, ACT, ADC, AFP, SAU, TLP na CCM na utaratibu wa kuwapatia ulinzi wagombea hao umeshaanza. Jecha alisema ofisi yake imeshafanya mawasiliano na vyama na wagombea na kuwapa taarifa mbalimbali za matayarisho ya uchaguzi, ili waanze taratibu za kupanga mawakala wao.
Alisema baadhi ya vyama vimetoa taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa havitashiriki katika uchaguzi, na kuwataka wagombea wao kuandika barua za kutoshiriki katika upigaji kura huo.
“Swala hili naomba nilitolee ufafanuzi kidogo kwa kuwa kauli za vyama hivyo zimewachanganya baadhi ya wagombea waliodhaminiwa na vyama hivyo, ambao bado wanataka kugombea katika uchaguzi huo,” alisema Jecha.
Alisema kila chama cha siasa kilichosajiliwa kinachokusudia kushiriki uchaguzi wa Rais kitawasilisha jina la mgombea wake wa urais kwa tume, na ili mtu awe ameteuliwa kihalali kuwa mgombea urais ni lazima awe amedhaminiwa kwa maandishi na watu wasiopungua 200 ambao wameandikishwa kuwa wapiga kura kutoka kila mkoa wa Zanzibar.
“Kwa bahati mbaya mpaka tunapowasilisha taarifa hii, hakuna chama hata kimoja kati ya vyama ambavyo vimejinadi kuwa havitashiriki katika uchaguzi kilichoiandikia Tume kuwa kimefuta udhamini wa wagombea wake kushiriki katika uchaguzi,” alisema Jecha katika taarifa yake.
“La pili ni kuwa utaratibu wa kujitoa kwa wagombea katika uchaguzi umefafanuliwa vizuri sana katika kanuni ya uchaguzi ya mwaka 2015,” alisema mwenyekiti huyo akisisitiza kuwa haukufuatwa.
Kwa mujibu wa vifungu hivyo, alisema mgombea wa urais anaweza kujiondoa kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoitia saini mwenyewe atakayoiwasilisha kwa mwenyekiti si zaidi ya saa 10 jioni siku ya uteuzi.
“Mgombea uwakilishi na udiwani anaweza kujiondoa kwa kutoa taarifa ya maandishi aliyoitia saini mwenyewe atakayoiwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi si zaidi ya saa 10 jioni ya siku inayofuatia siku ya uteuzi.
Jecha alifafanua kuwa tarifa ya kujiondoa chini ya kanuni hizo inatakiwa iambatanishwe na tamko la kisheria lililotolewa na kutiwa saini na mgombeya mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu kwa mgombea wa urais na hakimu kwa mgombea wa uwakilishi au udiwani, mambo ambayo hayakufanyika.
Kuhusu daftari la wapigakura, Jecha alisema kazi ya uchapishaji wa madaftari na vituo vya kupigia kura ndani na nje imeshakamilika, na wanatarajia mwisho wa mwezi huu majina hayo kubandikwa.
Alisema ratiba ya mafunzo kwa wasaidizi na wasimamizi wa majimbo imeshakamilika, na mafunzo hayo kwa Unguja na Pemba yataendeshwa Februari 22-28 na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo watapewa mafunzo Machi 2 hadi Machi 5.
Alisema mafunzo mengine yatakayotolewa ni ya wasaidizi wa vituo vya kupigia kuwa ambayo yamepangwa kufanyika Machi 11 -13 na mafunzo ya mawakala wa uchaguzi siku ya Machi 14 na mafunzo ya walinzi wa vituo vya kupigia kura Machi 15, 2016.
Jecha alisema kazi ya upangaji wa vifaa vya kupigia kura kwa ajili ya kusambazwa wilayani tayari imeanza katika ghala za ZEC za Unguja na Pemba na baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, utaratibu wa kuvisafirisha katika wilaya husika utaandaliwa.
Kuhusu uchapishaji karatasi za kura, mwenyekiti huyo alisema matayarisho yamekamilika baada ya tume kumpitisha mchapishaji wa karatasi hizo.
Chanzo: Mwananchi

Sekeseke jipya la Makonda na Meya kuhusu utendaji. huenda hukuipata hii





Paul Makonda
Paul Makonda: Mkuu wa wilaya ya Kinondoni 
 Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni,  Boniface Jacob na Mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda wameingia kwenye mvutano  kuhusu kuvuka mipaka ya utendaji wa halmashauri hiyo.
Mvutano huo umekuja baada ya Jacob  kumtuhumu Makonda kuwa ametoa  taarifa za kikao cha kamati za fedha ya halmashauri hiyo kilichofanyika wiki iliyopita kinyume na taratibu.
“…Tena hata kwenye kikao hakuwepo,  lakini nashangaa kuona ameenda kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa Wilaya ya Kinondoni inatarajia kupata dola 300 milioni za Marekani sawa na Sh600 bilioni kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alisema Jacob jana kwenye mkutano na waandishi wa habari.
“Vikao vyote vya halmashauri ni siri…huo ni upotoshaji na Makonda anaingilia mamlaka zisizokuwa za kwake, ” alisema.
Jacob alisema halmashauri hiyo imeshindwa kufumbia macho jambo hilo kwani linaweza kuleta mvutano baadaye.
“Mimi nalalamikiwa na wajumbe wa kamati, wanasema kwa nini taarifa za kikao ambazo ni za siri zinatangazwa wakati bado michakato yake inaendelea?” alihoji Jacob.
Meya huyo alisema Makonda ambaye alipewa taarifa hizo na maofisa tarafa waliohudhuria kikao hicho, alitakiwa kuuliza uongozi wa halmashauri kabla ya kutangaza kwa umma.
“Sasa leo ikitokea wajumbe wamegoma kupitisha maazimio  kuhusu mchakato huo  hizo hela atatoa wapi?” aliendelea kuhoji.
Alisema  endapo Makonda ataendelea na tabia hiyo,  maofisa tarafa watazuiliwa kuhudhuria kwenye vikao vya kamati za fedha za halmashauri hiyo.
Hata hivyo, Jacob alisema si mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa wilaya kuvuka mipaka na kuingilia shughuli za halmashauri, ambazo kimsingi zinapaswa kufanywa na meya, mkurugenzi au msemaji wa halmashauri.
Meya huyo alisema mara ya kwanza Makonda alisema  halmashauri itajenga machinjio ya kisasa, wakati anafahamu hana uwezo wa kupata fedha za kufanikisha mradi huo.
Jacob alisema  halmashauri ndiyo yenye dhamana na kuidhinisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Pili, aliwahi kuwaita wenyeviti wa Kinondoni Leaders Club kwa ajili ya kuzungumzia mchakato wa kuvunja maeneo ya wazi yaliyojengwa.
Kwa upande wake Makonda kueleza kuhusu madai hayo, alisema Jacob bado ni mwanafunzi hivyo hawezi kuzungumza chochote juu ya madai hayo.
“Amechaguliwa kuwa meya juzi tu bado mwanafunzi, hafahamu mipaka ya mamlaka yangu. Akijifunza na kuelewa hizo kelele hamtazisikia tena,” alisema Makonda.

Kuna habari ya mwanasheria wa Halmashauri kushonewa suti ya laki tano. nimekuwekea full story





Madiwani wa Halmashauri ya Mbeya Vijijini wamegoma kupitisha kifungu cha bajeti ya kumnunulia mwanasheria wa halmashauri suti ya Sh500,000 kila mwezi.

Awali, akiwasilisha bajeti ya mwaka 2016/17 kwenye Baraza la Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri Mbeya Vijijini, Mwanasheria Prosper Msivala alisema kila mkuu wa idara atapata Sh180,000 kwa ajili ya mawasiliano huku wanasheria wakipewa Sh500,000.
Msivala alisema suti ya mwanasheria ni pamoja na viatu, shati, suruali na koti pamoja na skafu yake.
Diwani wa Maendeleo Mbeya Vijijini, Daniel Mwanyamale alipinga mwanasheria kushonewa sare kila mwezi kwa Sh500,000.
Aliwataka waandaaji wa bajeti hiyo kuangalia upya suala hilo na kwamba hata suala la kupewa Sh180,000 za mawasiliano nalo halikubaliki.
Diwani Ramadhani Njelambaa alisema afadhali fedha hizo zipelekwe kwenye shughuli za maendeleo ukiwamo ujenzi wa madarasa na ununuzi wa dawa za vituo na zahanati.
Hata hivyo, Mwanasheria Msivala alitetea fedha hizo akisema ni jukumu la halmashauri kutoa na kuwaomba madiwani wapitishe.
“Ndugu zangu kila mwanasheria anapoajiriwa katika halmashauri yetu ni lazima kila mwanasheria apate Sh500,000 na hilo lipo kisheria,” alisema.
Mbunge wa Mbeya Vijijini, Aran Njeza aliwasihi madiwani kuachana na mijadala ya posho katika vikao badala yake wajadili matumizi ya fedha zilizopangwa kwa miradi ya maendeleo ya wananchi.