Wednesday 27 April 2016

Uhaba wa umeme wasababisha watumishi wa umma kufanya kazi siku kwa wiki Venezuela.



Serikali ya Venezuela imeagiza wafanyakazi
wake wawe wakifanya kazi siku mbili kwa wiki.Hii ni hatua ya muda iliyochukuliwa kutokana na uhaba wa umeme.

Makamu wa Rais Aristobulo Isturiz ametangaza kwamba watumishi wa umma wanafaa kufika kazini Jumatatu na Jumanne pekee hadi mzozo wa sasa wa nishati umalizike.

Venezuela imekabiliwa na ukame mkubwa ambao umepunguza maji kwenye bwawa lake kuu la kufulia umeme.



Lakini upinzani umeituhumu serikali kwa
kutodhibiti vyema mzozo wa sasa. Agizo la kupunguzwa kwa siku za kufanya kazi,
lililotolewa kupitia runinga ya taifa na Bw Isturiz.

"Hakutafanywa kazi katika sekta ya umma
Jumatano, Alhamisi na Ijumaa, ila tu majukumu muhimu sana.” alisema.

Amesema Venezuela imeathiriwa sana na hali ya hewa ya El Nino na kwamba hali ya kawaida itarejea baada ya mvua kuanza kunyesha.

Serikali imekuwa ikichukua hatua kadhaa
kupunguza matumizi ya umeme. Februari, maduka yaliagizwa kupunguza muda
ambao yanafunguliwa kila siku na pia kujaribu kujizalishia umeme.

Mapema wiki hii, serikali pia ilisongeza mbele saa kwa nusu saa ili kupunguza mahitaji ya umeme kwa ajili ya mwanga mapema jioni.

No comments: