Tuesday 26 April 2016

Watatu wakamatwa wakisafirisha Madawa Kilimanjaro


Watu watatu akiwemo mmoja raia wa Kenya
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa
ya kulevya aina ya Mirungi na Bangi kilo 54
na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa
kutoka nchini Kenya kwenda mkoani Arusha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro
Bw.Wilbrod Mutafungwa amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa katika
maeneo ya njia panda Himo wilaya ya Moshi
na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye
miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi
miguuni.

Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor
mfanyabiashara mkoani Arusha, Naftal Mvoyi
mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis
mkazi wa Arusha ambao walikuwa
wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia
magazeti na gundi ya karatasi na kisha
kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa
wakitokea nchini Kenya kuelekea jiji la
Arusha.

Ripota wetu amefanikiwa kuzungumza na
baadhi ya vijana wanaojihusisha na matumizi
ya madawa ya kulevya katika manispaa ya
Moshi na kueleza kwamba changamoto
kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali
inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na
matukio ya uhalifu.

Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri
vijana wengi kiafya kutokana na baadhi yao
kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na
hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya
wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

No comments: