Thursday 28 April 2016

Majengo 20 ya CCM Kubomolewa Moshi.


Ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kinyume na sheria za mipango miji katika Manispaa ya Moshi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Ubomoaji huo unakusudiwa kuambatana
na uvunjaji wa majengo zaidi ya 20 ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyopo katika Kata ya Mawenzi.

Meya wa manispaa hiyo, Raymond Mboya
amewaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kusimamia ipasavyo sheria hiyo ili kuhakikisha majengo yaliyojengwa kinyume na sheria yanavunjwa.

Mboya amesema sheria ni lazima ifuatwe
haijalishi ni chama gani kimejenga kinyume.

Leo tunapata ugumu wa kuwa jiji kutokana na sisi wenyewe kushindwa kusimamia sheria za mipango miji, hatuwatendei haki wakazi wa Manispaa ya Moshi ni lazima ifike wakati watu
tujue kuna mamlaka ambayo imekabidhiwa kusimamia mji,”amesema Mboya.

Kwa upande wake Loth Ole Mesele, Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini amesema hajapata taarifa hizo za kubomolewa kwa majengo ya chama hicho.

No comments: