Wednesday 9 March 2016

Harmonize ameweka bayana sababu za kuwa single

harmonizerr
Msanii wa bongo fleva Harmonize amesema kuwa toka aingie kwenye utu uzima hajawahi kujihusisha na mambo ya mapenzi kwa sababu anataka kufanya maamuzi sahihi ambayo hatayajutia.

akiongea kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Tv Harmonize amesema anataka apate mwenza ambaye atakayeweza kumtambulisha kwa jamii na ikamuelewa ndio maana yupo makini kwenye swala kama hilo.

Toka niingie kwenye utu uzima sijaingia kwenye mahusiano kwa sababu nataka nifanya maamuzi sahihi.Nataka nikiingia kwenye mahusiano niweke wazi kila mtu ajue” alisema msanii huyo anayetamba na wimbo wa bado.

Source: Clouds Tv