Wednesday 9 March 2016

JohMzava: Wizi wachelewesha mipango ya kundi


JohMzava mmoja wa member wa Kundi la A-Town Good Music. (Picha na Maktaba)

Msanii anayefanya vizuri kutokea Arusha Johmzava amesitisha kutoa kazi zake mpya pamoja Na za kundi baada ya kuibiwa baadhi ya vifaa vyake.    
Msanii huyo ambaye kwa sasa anaunda kundi la A TOWN GOOD MUSIC alipata mkasa wa kuibiwa Laptop, Simu mbili aina ya Nokia Na Samsung Galaxy Na pesa taslim shilingi laki 3.

Johmzava ameiambia BongoHomeTz kuwa vitu alivyoibiwa vina thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1 Na laki 9.
"Niliibiwa kwenye mazingira ya kutatanisha kiasi cha vitu Na pesa vyenye thamani ya kama milioni Na laki tisa Na NUSU hivi" alisema Johmzava.

Ameongeza kuwa tukio hilo limechelewesha kazi zao mpya zilizofanyika NoizMekah Production kwani mipango yote ilikuwa kwenye flash ambayo pia iliibiwa.

Amesema wao kama kundi la A TOWN GOOD MUSIC Linaloundwa na wakali wawili JohMzava na Ofty watahakikisha wanaziachia nyimbo zao mpya zilizofanyika NoizMekah Production kwani wana mipango ya kuwaridhisha mashabiki wao.


Johmzava alitambulishwa vyema Na Ngoma yake ya BORN TO WIN iliyofanyika LostPoetry chini ya Della P Na amesema kwa sasa anajipanga akiwa Na mwenzake wanaounda kundi la A TOWN GOOD MUSIC.