Saturday 19 March 2016

Ommy Dimpozz: Mwaka huu nitamtambulisha msanii katika Lebo yangu ya PKP

Ommy Dimpozz kwa poz Tanzania Musician 
Muziki wa Tanzania unaelekea kukua zaidi kutokana na mastaa kibao kuanzisha lebo zao kuwasaidia wasanii wanaochipukia.

Akizungumza na kipindi cha Friday Night Live,kinachoruka kupitia EATV, Ommy Dimpoz alisema mwaka huu atamtambulisha msanii mmoja kutoka lebo ya PKP kwa kirefu Poz Kwa Poz

Baada ya kuanzisha lebo yangu ya PKP, Mwaka huu kumtambulisha msanii wangu mmoja. Najua watu watasema kuwa mpaka fulani aanzishe na wewe ndio uige,Ila nilitangaza muda kuwa nimeanzisha lebo yangu.” Alisema Dimpozz

Ommy Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha Achia Body ambacho kwa sasa kina walau takribani miezi mitatu ivi.