Saturday 19 March 2016

Msanii Mwasiti Almas ameweka bayana mambo manne yanayomfanya avutie, Ugali na Dagaa vimo




Mwasiti akizungumza na EATV ametoa ya moyoni kuhusiana na mwonekano wake kwa sasa kuonekana anavutia zaidi tofauti na siku za nyuma.

''Kwa sasa nina mapenzi ambayo ni salama japo siwezi kumtaja Mpenzi wangu kwa sasa kwa sababu bado ni mapya ila nina faraja sana'' amesema Mwasiti

Pamoja na hayo Mwasiti amesema kwamba aina za vyakula kama ugali na dagaa na kupumzika sana hinachangia pia muonekano wake kuonekana wa kuvutia.

Ikumbukwe Mwasiti ni msanii wa kike mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni ambae amekamalia katika gemu ya muziki wa bongo. Pata futsa ya kuitazama video hii ya mwanadada Mwasiti.

Mwasiti ft Queen Darleen- Sema nae