Sunday 6 March 2016

Gundua kusudi la maisha yako ili ufanikiwe

vijana

Watu wengi duniani wanasumbuliwa na tatizo la kutokujua kwanini wapo duniani na wanatakiwa wafanye nini?
Wamejikuta wanafanya kazi ili walipe bili na kulipa kodi bila kujua kuwa maana ya maisha haishii kwenye kulipa bili ya umeme,maji,ada na kodi ya pango.Maana ya maisha inakwenda mbele zaidi ya hapo na haina mipaka ya namna hiyo.
Wako watu wanaofanya kazi ambazo hawazipendi na wanaenda kazini kila siku na kurudi nyumbani jioni ama usiku wamechoka huku wakiwapa mgongo wenzi wao wakati wa usiku kutokana na msongo wa mawazo,stress,maumivu na machungu waliyonayo wanashindwa kufurahia maisha.
Yote hayo ni Kwasababu wanafikiri wanaishi ili kulipa bili na kodi mbalimbali hawaoni cha zaidi katika maisha yao.
Matokeo yake wamejikuta wamekua watumwa wa fedha ,fedha zinawatumikisha mpaka mpaka wanasahau kuzitumikia ndoto zao na kutimiza kusudi la maisha yao.
vija2
Matajiri wengi hawafanyi kazi kwa ajili ya fedha,fedha zinafanya kazi kwa ajili yao na kuwazalishia fedha hivyo hana haja ya kutafuta fedha kwa sababu amejenga miundombinu za fedha hivyo fedha zinaflow kumfuata yeye na si yeye anazifuata.
Tengeneza mazingira ya kuzitumikisha fedha zikusaidie kutimiza ndoto zako ,maono na mawazo mazuri uliyonayo na si kuishia kufurahia kuwa unaweza kulipa bili na kodi bila kusumbuliwa.
Katika moja ya makala zangu nimewahi kuandika juu ya mvuto alionao mtu ambao unavuta fedha mithili ya sumaku fulani hivi,kwa maana ya kipaji,ubunifu na uwezo wa kipekee ambao unahitajika unaweza kuutoa ukabadilishana na watu wa kakupatia fedha.
Kwa maana fedha hupatikana kwa nguvu ya mbadilishano aidha bidhaa kwa fedha ama huduma kwa fedha ,na kila mtu amezaliwa ana bidhaa ama huduma iko ndani yake ambayo ni muhimu sana kwa jamii akianza kuitoa nje itahitajika na watu watamletea fedha wapate huduma yake.
Fedha zinakupenda na sio wewe unazipenda katika vitabu vitakataifu imeandikwa kwamba “Ukipenda sana fedha hutashiba fedha” pia imeandikwa “Mali ikiongezeka na walaji wanaongezeka “ kwa maana fahari ya tajiri inaweza kuishia kwenye macho yake wala asifahidi kwa kiwango stahiki.
Ni vizuri kuwa tajiri lakini ni vyema kuwa tajiri anayetimiza kusudi la maisha yake ,haina maana mtu kuwa na fedha nyingi alafu anaishi maisha ambayo hayana maana wala sababu.
Baada ya kupata fedha nyingi,jumba la kifahari na magari bado kuna swali linakujia kwanini uko duniani ilo ni swali la muhimu ambalo unapaswa kulijibu ili kutimiza kusudi la wewe kuwepo duniani na kuishi maisha yenye maana.
Ina maana gani kuishi maisha ambayo hayana maana ? ina maana gani kuwepo duniani na kutokujua sababu ya kuwepo duniani?

Mwandishi wa makala hii ni:
Ferdinand Shayo, Arusha

No comments: