Wednesday 2 March 2016

UNESCO: Wasichana bado wanakosa haki ya kupata elimu



Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake hapo Machi 8 takwimu  za  UNESCO kuhusu "usawa wa kijinsia katika elimu" zinaonyesha kwamba wasichana bado ni wa kwanza katika kunyimwa haki ya elimu licha ya juhudi zote zilizofanyika na hatua zilizopigwa katika miaka 20 iliyopita.

Ripoti inasema pengo la kijinsia ni kubwa hasa katika mataifa ya Kiarabu, Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na Kusini na Magharibi mwa Asia

Imeongeza kuwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wasichana milioni 9.5 hawatowahi kuhudhuria shule ikilinganishwa na wavulana milioni 5.

Kwa jumla watoto zaidi ya milioni 30 wa umri wa miaka 6 hadi 11 hawasiomi. Na pengo ni kubwa zaidi katika mataifa ya Kiarabu ambako asilimi 80 ya wasichana hawasomi ikilinganishwa na asilimi 16 ya wavulana.

Chanzo: Radio UM

No comments: