Wednesday 2 March 2016

Meda Classic aendelea kufanya media Tour ndani ya Arusha



Hit maker wa single ya Barua kwa Diamond Na Kongoi Meda Classic yupo Arusha Kwenye Media tour ya kutambulisha Ngoma yake Mpya inayokwenda kwa jina La Somebody.    

Mkali huyo anayewakilisha Mkoa wa Iringa tayari ameanza kufanya ziara yake kwenye Media mbali mbali mkoani Arusha.

Meda akiwa chini ya uongozi wa meneja wake Kibo Matthew au Mr Kibo ameshafanya ziara kwa kuanzia Tripple A FM siku ya Jana Na Leo jumatano amefanya Interview ndani ya Redio 5.  

Pamoja Na mambo mengine Meda ametoa shukran kwa mashabiki wake walioonyesha sapoti kubwa Na kuahidi kuwa video ya wimbo wake mpya Somebody itafanyika hivi karibuni.        
Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia blog ya BongoHomeTz, Meda Classic ataendelea kuitangaza kazi yake Mpya ndani ya Redio Stations za Mkoa wa Arusha.

Katika moja ya Mahojiano yake Meda amesema kuwa anawakubali mastaa kibao wa hapa Tz wakiwamo Diamond, Weusi, Navykenzo, Kassim mganga Na wengine wengi.

No comments: