Thursday 17 March 2016

Mo Town: Kukosa meneja kunaugharimu muziki wangu.

Msanii Chipkizi kutokea mkoani Kilimanjaro Mo Town Star (Picha na Maktaba)


Msanii Mo Town Star anayewakilisha vyema Mkoa wa Kilimanjaro amesema kwa sasa yupo studio akiandaa wimbo mpya.

Mo Town Star ameiambia BongoHomeTz kuwa kwa sasa anajipanga kutoa wimbo mpya ambao amesema anaamini mashabiki wake watapata ladha tofauti na waliyoizoea.

"Ni International song, ninafanya Na producer mkubwa Na pia Ni studio kubwa hivyo nategemea utakuwa wimbo mkubwa pia" alisema Mo Town Star.

Hata hivyo Mo Town Star ameongeza kwa kwa kueleza kuwa anachelewa kufanya kile anachofikiria kukifanya kutokana Na kujisimamia mwenyewe kwani hadi sasa hivi Hana meneja.

"Sina meneja, najisimamia mwenyewe Na nimeweza kupiga hatua kubwa, nahisi nikipata meneja nitafika ninapotaka kwa kuwa najiamini Na ninatambua ninachofanya" ni maneno ya Mo Town Star alipozungumza nasi.

Mo Town Kwa sasa anafanya vyema Na wimbo wake wa "Nikuache Uende" ambao umepokelewa vizuri Na Mashariki wake lakini pia anafanya vizuri Na nyingine kama Mapenzi Na wewe, Mapenzi Kamari Na nyinginezo.

Unaweza kudownload moja ya nyimbo za Mo Town star kwa kubofya HAPA KUDOWNLOAD Mo Town Star-Nikuache uende.