Saturday 5 March 2016

Waziri mkuu atoa siku kumi kwa viongozi wa wilaya ya Meatu

Waziri mkuu,Kassim Majaliwa ametoa siku kumi  kwa viongozi wa wilaya ya Meatu kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu kwenda sekondari wanakwenda sekondari na kwamba kama wakishindwa kufanya hivyo atawachukulia hatua.

Waziri mkuu ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwakaluba wilayani Meatu kabla ya kuzindua jengo la maabara la shule ya sekiondari ambapo amesema ameskitishwa na taarifa kuwa wanafunzi 589 waliofaulu  kwenda sekondari hawajaenda.
 
Aidha waziri mkuu amemuagiza mkuu wa wilaya hiyo na mkurugenzi kuhakikisha wanatenga pesa za kutosha za kununulia madawati ili wanafunzi wasipate shida ambapo amesema serikali inaompango wa kuajili waalimu 40,000 mwaka huu wakiwemo waalimu wa sayansi ambao watapeleka nchi nzima ikiwemo wilaya ya Meatu huku akiishukuru benki ya nmb kwa kuchangia katika elimu ambapo imekuwa ikitoa madawati mengi katika shule mbalimbali hapa nchini.
 
Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa waziri mkuu,mkuu wa wilaya hiyo,Erasto Sima amesema wilaya imedhamilia kuwapa kipaumbele wakulima kutoka jembe la mkono ambapo jumla ya matrekita  41,yameuzwa kupitia wakala wa SUMA JKT.
 
Akiwa wilayani Meatu waziri mkuu ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekita za kilimo ,elimu na afya ambapo pia amehutubiwa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stend mjini mwanuhzi.

Chanzo: ITV

No comments: