Thursday 3 March 2016

Mkubwa Fella: Nitagombea urais mwaka 2040.

Saidi Fella (picha na maktaba)

Fella ambaye pia ni meneja wa Yamoto band na TMK wanaume family ameyasema kuwa atagombea uraisi mwaka 2040 alipokuwa akizungumza na E News ya EATV.

''Kama Mungu akinipa uhai mwaka huo nitakuwa na miaka 60 na nitakuwa nina uelewa wa kutosha na uwezo wa kuweza kuwaongoza watanzania kwa kujali maslahi yao ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini'' Amesema Fella.

Aidha Fella ametamba kuwa yeye anafanya kazi kwa vitendo ndiyo maana wananchi wa kata yake walimuamini na katika madiwani wote wa Dar es salaam yeye ndiye diwani pekee aliyeshinda kwa asilimia 89% katika uchaguzi mkuu wa October 2015.

No comments: